Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe
Wanyama katika Mbuga za Tanzania..(Picha ya Maktaba).
Mwamko
mdogo wa Watanzania kutembelea hifadhi za Taifa zilizo katika maeneo
mbalimbali nchini umeathiri kiwango cha idadi ya watu wanaotembelea
hifadhi hizo kwa mwaka hivyo kuzorotesha mapato yanayotokana na watalii
wa ndani ya nchi.
Kauli
hiyo imetolewa Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Maliasili na Utalii
Prof. Jumanne Maghembe wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na
Matumizi ya Wizara ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017.
Amesema
kuwa licha ya Serikali kuweka gharama ndogo za viingilio katika hifadhi
za Taifa kwa watanzania na raia wa Jumuiya ya Afrika Mashariki bado
mwamko ni mdogo hasa idadi ya watanzania wanaokwenda kutembele hifadhi
hizo jambo linalopunguza mapato yanayotokana na utalii wa ndani wa
watanzania.
Ameeleza
kuwa kwa sasa watanzania kwa maana ya watu wazima wanaotembelea hifadhi
za ndani zilizoko eneo la Kaskazini hutakiwa kulipa kiingilio cha
shilingi elfu kumu (10,000) na shilingi elfu 5000 hadi 15,000 kwa
hifadhi zote zilizoko kusini mwa Tanzania huku watoto wakilipia shilingi
2000 kutembelea hifadhi yoyote nchini.
Prof.
Maghembe ameeleza kuwa kufuatia hali hiyo Wizara yake inaendelea na
kampeni mbalimbali ili kuwahamasisha Watanzania Wengi zaidi kushiriki
katika shughuli za utalii ndani ya nchi hivyo kuongeza patoa la Taifa.
Amesema
katika kulinda na kutunza hifadhi za Taifa ili kuhakikisha zinakuwa
endelevu na kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa, Serikali ya
awamu ya tano imejipanga kikamilifu ujangili wa wanyama pori kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali wa uhifadhi.
Amefafanua
kuwa katika kupambana na ujangili nchini Wizara kwa kushirikiana na
wadau wa uhifadhi imeshawabaini na kuwashughulikia baadhi ya wananchi
wanaoishi kwenye maeneo yanayopakana na hifadhi wanaoshirikiana na
watumishi wasio waaminifu kushiriki vitendo vya ujangili pia
kuwashughulikia wawindaji haramu wanaojihusisha moja kwa moja kuua
wanyama kufanya udalali na kusafirisha wanyama hao.
Aidha,
amesema kuwa katika kupambana na ujangili Serikali inaendelea kufanya
doria ili kuwashughulikia wawezeshaji ngazi ya nchi wanaonunua nyara,
kusambaza silaha, watakatishaji fedha , majangili nguli wa kimataifa kwa
kukitumia na kukiimarisha kitengo cha Intelijensia ili kiweze kutimiza
majukumu ya kiulinzi kwa ufanisi zaidi.
Pia
amesema kuwa Wizara hiyo imeendendelea kuongeza idadi ya askari
wanyamapori 447 na maafisa 111 na kufanya idadi ya watumishi waliopo kwa
sasa kufikia 2,064 pamoja na kuanzisha kada nane za doria za
ushirikiano katika mifumo ya ikolojia ya Selous-Niassa-Mikumi, Ruaha-
Ruangwa, Katavi -Rukwa , Moyowosi -Kigosi, Tarangire- Manyara-Simanjiro
na Ngorongoro – Serengeti.
Na. Aron Msigwa – MAELEZO-Dodoma.
0 maoni:
Chapisha Maoni