MBUNGE wa Jimbo la majinga Mjini, Cosato Chumi akikabidhi gari la Wagonjwa
(ambulance) kwa wananchi
(ambulance) kwa wananchi
Gari la wagonjwa [Ambulance] lenye thamani ya mill.40 lakabidhiwa
katika Hospitali ya wilaya ya mafinga na mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato
Chumi katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana kwenye viwanja vya mashujaa
mjini mafinga mkoani Iringa.
Chumi alikabidhi gari
hilo ikiwa ni moja ya ahadi yake alyoitoa wakati akiomba kura kwa wananchi wa
jimbo hilo katika kampeni ya uchaguzi mkuu 2015,ambapo alisema kutokana na
changamoto ya uhaba wa gari ya kubebea wagonjwa katika hosipitali hiyo, endapo
atapewa ya kuwa mbunge atahakikisaha
gari ya wagonjwa linapatikanaili wagonjwa waweze kufika hospital kwa wakati.
Akizungumza na wananchi wakati wa kukabidhi gari
hilo,mbunge Chumi alisema muda wa kupiga
siasa umeshapita na kazi iliyopo hivi sasa ni kuwaletea wananchi maendeleo kwa
kuwatatulia changamoto zinazowakabili.
Alisema pamoja na kuongeza gari ya wagonjwa atahakikisha
anaboresha vituo vya Afya vilivyopo
katika jimbo lake ili kupunguza wimbi kubwa la msongamano wa wagonjwa wanaokuja
kutibiwa Hospitalini hapo.
‘’’Nipo kwenye mchakato wa kuboresha vituo vyote vya Afya
ndani ya jimbo langu,na nitahakikisha huduma muhimu zinapatikanaikiwa pamoja na
dawa za kutosha na vifaa mbalimbali vinavyohitajika ili wananchi wangu waweze
kuhudumiwa bila usumbufu katika vituo hivyo,hii itasaidia kupunguza msongamano
katika hospitali ya wilaya’’’’’alisema chumi
Aidhakatika mkutano huo mbunge alisisitiza swala la uaminifu
kwa watumishi waliopewa dhamana ya kuwatumikia wananchi wahakikishe wanajikinga
na vitendo vinavyoashiria rushwa ,vinavyoweza
kuwaharibia sifa ya utendaji kazi zao na kushindwa kuwajibika ipasavyo katika
majukumu yao.
‘’’Sisi wabunge,madiwani na mtumishi yeyote aliyepewa
dhamana na wananchi anatakiwa ajiepushe na swala zima la rushwa ili aweze
kutenda haki kwa kuwatatulia changamoto wananchi wake waliomchagua. Tunatakiwa tuwatumie wananchi kuwaletea
maendeleo ipasavyo na si vinginevyo’’’alisema
Innocent Mhagama ni kaimu Mganga mkuu wa Hospitali ya
Wilaya mafinga,akipokea msaada wa gari
hilo kutoka kwa mbunge Chumi alisema gari hilo litaweza kusaidia kuokoa vifo vya wanamafinga hasa
mama na mtoto ambapo hapo awali kuliwa na gari moja tu.
Mhagama alisema kutokana na uwingi wa wagonjwa wanaoenda
kutibiwa katika hospitali hiyo kwa mwezi ni zaidi ya500 aliosimia kubwa ni
akina mama wajawazito na wengi wao wanafikishwa wakiwa katika hali mbaya kutokana
na gari la wagonjwa kuwa moja na kushindwa kumudu.
‘’’’Hospitali ilikuwa na gari moja tu la wagonjwa ambalo
lilikuwa linahudumia zaidi ya vituo 19 vilivyopo.Tunamshukuru mbunge kwa
kuliona hili na na kuokoa maisha ya watu hasa mama na mtotoingawa bado hitaji
lipo kutokana na uwingi wa wagonjwa endapo
tutapata gari la tatu itasaidia sana’’’’’alisema
Wananchi nao walitoa malalamiko yao kwa mbunge Chumi,ambapo
Maria Kanyika alimuomba mbunge aweze kusiomamia swala la utapikananji wa vibali
vya kuvuna miti,kwa kumtaka ahakikishe wazawa wa eneo husika wanapewa
kipaumbele ili waweze kunufaika mali alisi hiyo ilipo kwako.
‘’’’Tumelia
kwa muda mrefu,sisi tunanyanyasika kwa kuwapendelea wageni na kutuacha sisi
wenyeji tuliopo hapa.Nimeomba mara tano hivi sasa na ukizingatia mimi ni mjane
lakini naachwa na pesa yangu inaliwa
wageni wanapewa hali inayotukatisha tama wananchi tuliouzunguka msitu huu.’’’’alisema
0 maoni:
Chapisha Maoni