Halmashauri ya Manispaa ya
Iringa imewataka wakazi wa Mji huo kulipa kodi ya majengo na ushuru wa manispoaa
hiyo kwa hiyari ili kuinua uchumi wa Halmashuari hiyo inayojipanga kufikia
hadhi ya kuwa jiji
Kauli hiyo ilitolewa Meya
wa Manispaa hiyo Alex Kimbe alipokuwa akifunga kikao cha baraza la madiwani kilichokuwa
kikipokea taarifa za roba ya tatu ya mwaka kilichofanyika juzi kwenye ukumbi wa Mansipaa hiyo mjini hapa.
Kimbe alisema kwa
kipindi cha mizei mitatu Halmashauri hiyo imekusanya Sh 9,278,106,404 kati ya
makisio ya kukusanya sh 11,278,561,183,kwa kipndi cha miezi mitatu.
“Sisi Manispaa tumefanya
uthamani wa Majengo yote na niwaomba tu wananchi wa Iringa mlipe kodi ya
majengo na ushuru wa Masniuspaa kwa hiyari kwa kiwango mtakachoelezwa na
wataalamu wetu,hii itatusaidia kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwamo
afya,miundombinu na elimu”alisema Kimbe.
Awali baraza hilo
la madiwani lilipkea taarifa za
utekeelzaji wa miradi yamaendeleo kwa kipindi cha miezi mitatu ya robo ya tatu
ya mwaka na kusisitiz aumuhimu w awatendaji kuongez kasi ya utekelezaji wa
miradi hiyo.
Diwani wa kata ya
Mivinjeni Frank Nyalusi alisema ni muhhimu kwa watednaji kuhakiksha miradi
mbalimbali yamaendeleo inatekelezwa kwa wakati ili wananchi waweze kunufaika
nayo.
Mkuu wa wilaya ya Iringa
Richard Kasesela alishauri madiwani hao
kubuni njia mpya ya kukusanya mapato zisizo waumiza wananchi.
Kasesela alitoa mfano wa uboreshaji wa gereji bubu na
vituo vya kuoshea magari akidai maeneo hayo yanawea kusaidia kuongheza mapato na
hata kujenga kituo cha ukaguzi wa magari ambacho kingetumika pia kuongeza
kipato.
Katika kikoa hicho Kasesela amesitiza suala mipango
miji endelevu yenye kufikiria mbali zaidi, nyumba zote ambazo hazifai kwa
makazi wahusika waambiwe ili waweze kuziboresha huku akitaka Vichoro vyote vilivyo fungwa vifunguliwa ili
kuondoa hali hatarishi.
0 maoni:
Chapisha Maoni