Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akizungumza na wandishi wa habari
Mkuu wa wilaya ya
Iringa Richard Kasesela awaonya walimu wanaofanya mapenzi na wanafunzi wao wa kike katika shule
mbalimbali za msingi na sekondari wilayani Iringa.
Akizungumza na wanahabari
juzi ofisini kwake Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela alisema amepokea
taarifa za kusikitisha zinazowahusisha baadhi ya walimu katika shule zilozopo
manispaa ya Iringa kufanya mapenzi na watoto ambao ni wanafunzi na kusema kuwa
hali hili inasikitisha.
Kasesela alisema
baadhi ya wanafunzi hao wanafanya mapenzi na walimu wao kwa kulazimishwa na
kubakwa huku wakipewa vitisho mbalimbali vikiwemo vya kufelishwa mitihani yao.
Alisema Kamati ya
Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo kwa kushirikiana kwa jirani na jeshi la Polisi
imeanza kuzifanyia kazi taarifa hizo.
Alisema walimu
watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo watachukuliwa hatua za kinidhamu na
kisheria kwa mujibu wa sheria za utumishi na nchi.
“Tayari tumeanza
kazi ya uchunguzi wa taarifa hizo katika shule tatu kati yake mbili za mjini na
mmoja ipo Iringa Vijijini,” alisema bila kuzitaja shule hizo ili kutovuruga
ushahidi.
Alitoa wito kwa
wanafunzi wanaolazimishwa na walimu hao kufanyiwa vitendo hivyo kutoa
ushirikiano kwa kutoa taarifa za siri katika ofisi yake au Polisi.
“Huu ni
udhalilishaji mkubwa, hatuwezi kuwavumilia walimu wenye tabia kama hizo na
tutajitahidi kupata taarifa zao na kuwachukulia hatua ili kutoa fundisho kwa
wengine,” alisema.
Aliwataka wazazi na
walezi wa wanafunzi kuzingatia jukumu lao la malezi bora kwa watoto wao ili
kuwaepusha na vishawishi vinavyowza kuwaingiza katika matukio yanayoweza
kuwaharibu kitaaluma na kimaisha.
0 maoni:
Chapisha Maoni