Majenerali
na Wakuu wa Majeshi ya nchi kavu Barani Afrika wamekutana jijini Arusha
kujadili changamoto zinazoyakibili majeshi hayo ikiwemo tishio la
ugaidi, biashara ya madawa ya kulevya suala linalopelekea majeshi hayo
kuunganisha nguvu katika kupambana na matukio hayo.
Mnadhimu
Mkuu wa Jeshi Luteni Jenerali Venance Mabeyo amesema kuwa majeshi ya
nchi za Afrika kwa kushirikiana na jeshi la Marekani lenye teknolijia
kubwa iwapo watashirikiana na Majeshi ya Afrika kupambana na tatizo la
ugaidi na kufanikiwa
Katibu
Mkuu wa Wizara Ulinzi na Majeshi Job amesema kuwa jeshi la Tanzania
limejipanga kukabiliana na vitendo vya ugaidi ambavyo kwa nchi ya
Tanzania jukumu hilo linafanywa na jeshi la polisi kwa kushirikiana na
vyombo vingine.
Mnadhimu
wa Jeshi Marekani Jenerali Mark Milley pamoja na Balozi wa Marekani
nchini Mark Childress wamesema kuwa Marekani inasubiri kupata mawazo
mapya kutoka kwa majeshi ya Afrika juu ya namna ya kuimarisha uwezo na
nguvu za kukabiliana na changamoto za kiusalama.
Wakuu
wa Majeshi ya nchi Kavu wamekutana jijini Arusha kujadili juu ya
changamoto zinazoyakabili majeshi hayo ,na kubadilishana uwezo ili
kuwawezesha kupiga hatua katika mapambano dhidi ya ugaidi,madawa ya
kulevya,usafirishaji wa binadamu pamoja na uhalifu.
Imeandaliwa na Woinde Shizza, Arusha.
0 maoni:
Chapisha Maoni