Katika
kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya Uanuwai wa Utamaduni
Duniani Serikali imeitaka jamii kuhifadhi kulinda na kuheshimu utamaduni
wa nchi kwa vile ndio kitambulisho cha Taifa letu ili kuweza
kutambulika ndani na nje ya nchi.
Wito
huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya
Utamaduni kutoka Wizara ya Habari,utamadunu,Sanaa na Michezo Bi.Lily
Beleko wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu cha maadhimisho
ya siku ya Uanuwai wa Utamaduni Duniani ambapo kauli mbiu ya madhimisho
ya mwaka huu ni” Utamaduni wa Uadilifu na Nidhamu ya Kazi Huleta
Maendeleo”, “Sasa Kazi Tu”.
Kaimu
Mkurugenzi wa Utamaduni Bi.Lily Beleko amesema kuwa ni wajibu kwa kila
mtanzania kuheshimu Utamaduni wetu na kushiriki kikamilifu katika
kuutambua, kuujenga, kuuendeleza na kuurithisha kwa vizazi vingine.
“Siku
hii ni maalumu kwa kila mtanzaniana na kila mmoja hana budi kukubaliana
na harakati hizi za kulinda, kuhifadhi na kuendeleza Utamaduni wetu kwa
ajili ya vizazi vijavyo”Alisema Bi Lily.
Bi.Lily
Beleko ameongeza kuwa nchi haiwezi kutambulika na kuheshimika kama
Taifa huru bila kuwa na Utamaduni wake hivyo kuwepo kwa maadhimisho haya
kunaipatia jamii fursa ya kuendelea kukumbushana ,kuhamasishana na
kuhimizana katika kuuenzi utamaduni wa nchi.
Siku
ya Uanuwai wa Utamaduni Duniani huadhimishwa kila ifikapo tarehe 21
Mei, ambapo siku hiyo imeteuliwa na Baraza kuu la Umoja wa Mataifa
kuona umuhimu wa kuhifadhi na kuendeleza Utamaduni na hivyo kupitisha
Azimio Na 57/249 mnamo mwaka 2002.
Na Shamimu Nyaki
0 maoni:
Chapisha Maoni