Jumanne, 24 Mei 2016

Jamii yahimizwa kuwatunza vizuri wanyama wafugwao

indexNa Mahmoud Ahmad ,Arumeru
JAMII hapa nchini imehimizwa kuhakikisha kuwa inawapa matunzo mazuri
wanayama wafugwao,ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa inawapatia lishe
bora,makazi mazuri na kuwapatia huduma za afya.
Kaimu ofisa mifugo wa Halimashauri ya Wilaya ya Meru,Dkt.Asha Ali
aliyasema hayo juzi alipokuwa akifungua mafunzo ya namna ya kuwatunza
mifugo,kwa wanafunzi wa vyuo mbalimbali ya mifugo kutoka maeneo
mbalimbali hapa nchini.
Mafunzo hayo ya wiki moja ambayo yalilenga kuwapatia mbinu bora za
utunzaji wa waqnyama, yaliratibiwa na shirika la kuhudumia wanyama
Meru(MAWO) kwa ufadhili wa shirika la wanyama la WTG la Ujerumani
yalifanika katika Kata ya Kikatiti wilayani hapa
.
Wanyama waliolengwa  katika mafunzo hayo ni wale ambao wanaonekana
kutokupewa kipaumbele katika jamii licha ya umuhimu wao kwa jamii
ambapo wanayama hao ni punda paka na mbwa.
Dkt.Ali ametoa wito kwa wanachuo hao kuhakikisha kuwa wanazingatia na
kushika kwa makini yale yote wanayofundishwa ili waweze  kutumia ujuzi
huo kuelimisha jamii mbinu mbalimbali za kuwatunza wanyama hao.
Kwa upande wao wakufunzi wa mafunzo hayo,Dkt. Solomon Onyango na
Dkt.Amos Suppet kutoka taasisi Donkey Sanctuary ya Kenya(DSK),wamesema
kuwa katika mafunzo hayo wanachuo hao watafundishwa namna ya kuboresha
maisha ya wanyama ikiwa ni pamoja na kukabiliana na magonywa ya
mifugo.
Kadhalika wakufunzi hao wametoa wito kwa jamii kuhakikisha kuwa
wanawahudumia vizuri punda kutokana na umuhimu wao wa kubeba
mizigo,kutokuwapiga sana na kuhakikisha kuwa wanawatandikia tandiko
mgongoni ili wasiweze kuchumbuka na kupata vidonda pindi wabebeshapo
mizigo.
Kwa unde wake mratibu wa mafunzo hayo kutoka shirika la MAWO.Johnson
Lyimo amesema kuwa mpaka sasa Shirika lake kwa kushirikiana na WTG la
Ujerumani wameshatoa mafunzo hayo kwa wanachuo zaidi ya miambili
kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini.
Pia tumekuwa tukizunguka katika vijiji mbalimbali hapa nchini ambapo
tumekuwa tukitoa elimu hii kwa wafugaji ikiwa ni pamoja na kuitibu
mifugo hiyo hususani punda ambao tumewakuta wakiwa na magonjwa
mbalimbali.Na Mahmoud Ahmad ,Arumeru

mbalimbali.

0 maoni:

Chapisha Maoni