Wakala
wa Vipimo kwa kushirikiana na Mamlaka ya Serikali za Mitaa inakusudia
kuanzisha vituo maalum vya ununuzi wa mazao ya wakulima (buying
centres) katika vitongoji nchi nzima ili kuondoa unyonyaji na
ukandamizaji unaofanwa na wachuuzi wa mazao ya wakulima.
Kauli
hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Waziri wa Viwanda,Biashara na
Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage wakati akijibu swali la Mbunge wa Mlalo
Mhe. Rashid Shangazi aliyetaka kujua ni lini Serikali itasimamia sheria
kuondoa unyonyaji unaofanywa na wachuuzi wakati wa kununua mazao ya
wakulima.
Alisema
kuwa katika kutekeza hayo hakuna mfanyabiashara atakayeruhusiwa
kusafirisha mazao ambayo yamefungashwa kinyume kinyume cha Sheria ya
vipimo na kuongeza kuwa katika kusimamia jambo hilo vitaanzishwa vituo
maalum vya ukaguzi bila kusabaisha usumbufu katika ufanyaji biashara.
Mhe.
Mwijage amewaagiza Maafisa Ugani walioko vijijini watumike kusimamia
matumizi ya vipimo rasmi katika vituo hivyo na kutoa taarifa zote muhimu
kwa Wakala wa Vipimo.
Aidha
,alisema kuwa Serikali imeamua kufanyia mapitio Sheria ya Vipimo sura
340 ili kuondokana na unyonyaji na ukandamizaji unaofanywa na wachuuzi
wa mazao ya wakulima.
Alisema
kuwa Serikali imeamua kufanyia mapitio ya Sheria hiyo ili kuweka
mazingira mazuri kwa lengo la kumlinda muuzaji kwa kuwadhibiti manunuzi
wanaotumia njia za udandanyifu wakati wanaponunua mazao ya wakulima.
Mhe.
Mwijage alisema kuwa katika kipindi kifupi kijacho Serikali itawalisha
mabadiliko hayo bungeni ili ifanyiwe marekebisho yanayostahili.
Aidha
, Waziri huyo alisema kuwa pamoja na marekebisho ya Sheria ya Vipimo
yanatarajia kufanywa , Wakala wa Vipimo imewasilisha Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) mapendekezo ya kutungwa
kwa sheria ndogo(by laws) ili ziweze kuwaongoza wakulima na
wafanyabiashara kufungasha mazao.
0 maoni:
Chapisha Maoni