Kiongozi
wa zamani wa upelelezi nchini Uingereza amesema operesheni kubwa zaidi
zinahitajika maeneo ya mwambao wa Afrika ya Kaskazini kwa lengo la
kuondoa mgogoro wa wahamiaji haramu wanaoingia Ulaya.
Richard
Dearlove ambaye alikuwa kiongozi katika shirika la Uingereza la
Upelelezi amesema kuwa operesheni hizo zinaweza kuanza mara moja uwapo
mazingira ya kisiasa nchini Libya yataruhusu Umoja wa ulaya kufanya kazi
zake katika eneo hilo.
Katika
mazungumzo yake na BBC amesema kuwa mchakato unaoendeshwa na umoja wa
ulaya katika kukabiliana na suala hilo kuwa upo taratibu sana na sio wa
uhakika,huku akitoa onyo la ongereko la watu Ulaya kama watashindwa
kuzuia wahamiaji hao.
Pia
amekosoa mpango wa EU wa kutoa hati ya usafiri (visa) bure kwa raia wa
Uturuki wa kuingia na kutoka Uturuki bure na kuacha wahamiaji kwenda
Ugiriki.
|
0 maoni:
Chapisha Maoni