Alhamisi, 26 Mei 2016

BIMA YA AFYA KUANZA HUDUMA YA MAMA NA MWANA

NH1Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko Bw Bernard Konga, akitoa
salamu za Mfuko kwa wajumbe wa baraza hilo lilikofanyika katika ukumbi
wa Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro
NH2Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko Bw Bernard Konga,(katikati)
akizungumza na baadhi ya wajumbe ndugu Gudluck Kirambe, kulia na
meneja wa mkoa wa Kilimanjaro ndugu Fidelis Stephen.
NH3Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Mfuko wa Taifa wa Bima
ya Afya (NHIF) wanaohudhuria kika
NH4Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Mfuko wa Taifa wa Bima
ya Afya (NHIF) wanaohudhuria kika
NH5Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Mfuko wa Taifa wa Bima
ya Afya (NHIF) wanaohudhuria kika
……………………………………………………………………………………………………………………..
Kilimanjaro MFUKO wa taifa wa bima ya afya (NHIF) utaanzisha huduma mpya ya itakayojulikana kama mama na mwana afya kadi ili kuboresha huduma za bima ya afya kwa kundi hilo ambalo lipo katika uhitaji maalum.
Kauli hiyo imetolewa mjini hapa na kaimu mkurugenzi mkuu wa mfuko huo, bw Bernard Konga alipokuwa akitoa salamu za Mfuko huo kwa wajumbe wa baraza hili linaloanza kikao chake mjini hapa.
Bw konga amesema lengo la huduma hiyo mpya ni kuwawezesha kina Mama Wajawazito na Watoto kupata huduma za matibabu za uhakika zitolewazo na mfuko wa taifa wa Bima ya afya.
Chimbuko la hatua hiyo linafuatia matokeo mazuri na mafanikio makubwa ya mradi unaoendeshwa kwa pamoja kati ya NHIF na benki ya maendeleo ya ujerumani ya KfW katika mikoa ya Tanga na Mbeya. hatua iliyofikiwa kwa sasa ni kupata maoni ya wananchi kabla ya kuanza utekelezaji wake katika mwaka wa fedha wa 2016/17.
Awali, akifungua kikao cha baraza hilo, mkuu wa wilaya ya Siha Dr Charles Mlingwa, aliyemuwakilisha mkuu wa mkoa huo Meck Sadiki, aliushukuru mfuko huo kwa kuwa wabunifu katika utoaji wa huduma kwa makundi mbalimbali kwa kuzingatia uwezo wao wa kulipa. Ameutaka mfuko huo kutafsiri hotuba za mheshimiwa Rais kuhusu dhana ya afya bora kwa wote kwa kuweka mikakati katika eneo hilo.
Dr Mlingwa pia amesema wilaya ya Siha ni moja ya wilaya zilizofanikiwa sana kuboresha huduma za matibabu ambapo kwa miaka miwili mfululizo imeweza kupunguza sana vifo wa watoto wachanga na kufikia mtoto mmoja kwa kila watoto laki moja.

0 maoni:

Chapisha Maoni