Jumanne, 24 Mei 2016

VIJANA WATAKIWA KUACHANA NA UTUMIAJI WA MADAWA YA KULEVYA

Muandaaji wa tamasha la michezo kwa vijana wa mkoa wa Arusha Neema Mollel ambaye pia ni  Mwenyekiti wa CCM Kata ya Sakina pamoja na  mlezi wa Timu za mpira kata ya Sakina Jijini Arusha akiongea katika fainali za Tamasha la vijana lililofanyika katika viwanja vya kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid jijini hapa.
 
Martini Shimweta( Mdau) ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa  Olmatejoo A.
 
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Arusha Mjini Wilfred Soilel.
Diwani wa kata ya Ungalimited akiwa anawaasa vijana kuachana na madawa ya kulevya katika fainali hizo
 
Kiongozi wa Intersport Club akipokea kombe baada ya ushindi.
 …………………………………………………………………………………………………
Na Woinde Shizza,Arusha
 
Timu ya Intersport Club yaibuka kidedea katika Tamasha la vijana  mara baada ya  kuifunga Club ya mairiva bao 3 kwa 1 katika fainali iliyofanyika katika uwanja wa Shekhe Amir Abeid uliopo Jijini Arusha.
 Tamsha hilo ambalo lilianza mapema mwanzoni mwa mwezi huu limeweza kufikia tamati huku vijana wakiwatoa wito kwa wadau mbalimbali wa michezo kujitokeza kuanzisha mashindano kama haya kwani yanawasiadia kwa kiasi kikubwa 
Akizungumza wakati wa fainali za mashindano hayo muuandaaji wa mashindano hayo ambaye ni mwenyekiti wa CCM kata ya Sakina Neema Mollel alisema kuwa lengo la kuanzisha tamasha hili la vijana ni kuwaleta pamoja vijana na kuwapa elimu  ya jinsi ya kupiga vita utumiaji wa madawa ya kulevya kwa vijana 
Alisema kuwa vijana wengi wamekuwa wanajishirikisha na utumiaaji wa madawa ya kulevya ivyo aliona ni bora akatumia muda huu kuwaleta pamoja ili kuwapa elimu pamoja na kuwashirikisha katika tamasha hili la michezo ambalo limeweza kuwafundisha vijana wengi huku wengine wakiwa wameamua kuaachana kabisa na kutumia madawa haya ya kulevya badala yake wameamua kushiriki katika mazoezi pamoja na michezo
 
 “nia alisi ya  kuandaa mashindano haya ni kuwaleta kwa pamoja vijana pamoja na kupiga vita madawa ya kulevya kwa vijana,kuwaleta vijana pamoja,kuwaondoa vijana wasiendelee kukaa mitaani bila kazi kwani michezo ni ajira”Alisema Neema Mollel
 
Aidha aliwataka wazazi na jamii kwa ujumla kuwajengea vijana misingi Imara ilikuwajengea mtizamo mzuri wa maisha ya mbeleni badala ya kuwatupia lawama ambazo baadae zinajenga uadui kati yao na wazazi na
jamii.
 
Akikabidhi kombe kwa washindi ambao ni Interspot Club ,mwenyekiti wa CCM wilaya ya Arusha Wilfred Soilel amesema kuwa Michezo hujenga hujenga urafiki kati ya vijana ,wanafahamiana pia afya ya mwili inaimarika, pia itamfanya kijana ufahamu wake kuchangamka.
 
Sambamba ugawaji wa zawadi katika fainali hizo mshindi wa kwanza Intersport club kutoka kata ya Ungalimited, amekabidhiwa Kombe pamoja na  Tsh 100,000 ,Mshindi wa pili Mairiva club Tsh 75,000 na mshindi wa tatu ni Black Eagle Tsh 50,000.

0 maoni:

Chapisha Maoni