Jumanne, 24 Mei 2016

‘TUNASAKA’ NYOTA WAPYA– Mbeya City Council FC

DSC_0301
SIKU  chache baada ya pazia  la ligi kuu ya soka Tanzania  bara kufungwa,Kocha mkuu wa Mbeya  City Fc  Kinnah Phiri ameanza zoezi maalumu la kusaka nyota wapya ambao atawajumuisha  moja kwa moja kwenye vikosi vya timu yake  msimu ujao.
Akizungumza muda mfupi baada ya majaribio ya siku ya kwanza  kwa wachezaji wapya vijana waliofika kujaribu bahati zao kwa kuonyesha  vipaji walivyonavyo navyo, afisa habari wa City Dismas Ten amesema kuwa muitikio umekuwa mzuri katika siku hii kwanza ambayo nyota hao wa baadae wamefika kuonysha  uwezo wao mbele ya kocha huyo raia wa malawi.
“Leo ni siku ya kwanza, kitu kizuri mwitikio umekuwa mkubwa, takribani vijana 50 wamejitokeza kujaribu  bahati zao kulingana na vipaji walivyonavyo, haya ni majaribio ambayo kocha Phiri ameyaitisha ili kusaka vipaji vipya ambavyo moja kwa moja vitaingia kwenye timu yetu kubwa na ile ya U20, alisema.
Akiendelea zaidi, Ten  alisema kuwa,  hii  imekuwa ni kawaida kwa City kila inapofika mwisho wa msimu kuwaleta  pamoja vijana wote wanaoamini wanauwezo wa kucheza mpira, kufichua  vipaji vyao ili waje kuwa wachezaji wakubwa  baadae.
“Hii ni kawaida yetu, kila tunapomaliza msimu huwa tunafanya hivyi, vijana wote wenye umri kuanzia miaka 17-22 ni fursa kwao kujitokeza, zoezi hili la kusaka vipaji  litakuwepo kwa juma zima, leo hatukuwa na kocha Phiri kwa sababu  alikuwa kwenye majukumu mengine lakini kesho tutakuwa  kwenye uwanja Sokoine na mwalimu  atakuwa, kwa hiyo vijana wote ndani ya jiji la Mbeya na mikoa ya jirani waje kujaribu bahati zao.
Kwa upande wa vijana waliojitokeza siku ya leo, walishukuru kuwepo kwa zoezi hili kwa sababu limerahisisha  uwezekano wa vipaji walivyonavyo kuonekana mapema hatimaye waweze kutimiza ndoto zao za kuwa wachezaji wakubwa  siku za usoni

0 maoni:

Chapisha Maoni