Nchi
25 ikiwemo Marekani zimekubaliana kuipa silaha serikali ya Libya kwa
lengo la kuiwezesha kukabiliana na wanamgambo wa IS wanaoendelea
kuisumbua nchi hiyo.
Muungano
wa kimataifa umesema kuwa utalegeza vikwazo vya silaha vya Umoja wa
Mataifa juu ya Libya kutoa silaha kwa vikosi vinavyounga mkono serikali
mpya ya Tripoli.
Waziri
mkuu wa Libya Fayez al-Sarraj, amesema kuwa IS wamekuwa kikwazo kikubwa
sana kwa nchi yake na msaada huo wa kimataifa utakuwa muhimu katika
kupambana na ugaidi kwa mafanikio.
Nchi
hizo tano ambazo ni wanachama wa kudumu wa baraza la usalama la umoja
wa mataifa walifikia makubaliano hayo baada ya mazungumzo mjini
Vienna.Libya imekumbwa na machafuko tokea kuangushwa kwa kanali Gaddafi
mwaka 2011.
|
0 maoni:
Chapisha Maoni