Kaimu katibu
wa chama cha mapinduzi ccm mkoa wa Iringa
ambae pia ni katibu wa ccm Iringa Mjini mkoani hapa, Elisha Mwampashi
amewataka amewataka watanzania kuunga
mkono juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano kwa vitendo ili Taifa
liweze kupiga hatua kimaendeleo
Akizungumza
leo[jana]na wananchi jamii ya wafugaji ambao ni wamasai wakati akifungua shina la kijiwe cha
wakeleketwa ccm katika kitongoji cha Mahove kata ya mauninga jimbo la Isimani
Halmashauri ya Iringa kilichojengwa na wamasai kwa lengo la kuunga mkono kazi
mbalimbali zinazfanywa na mh. Rais dkt Magufuli na serikali yake.
Mwampashi
alisema kauli mbiu iliyoandikwa katika
kijiwe hicho ya Hapa kazi tu inatakiwa
kuungwa mkono kwa vitendo kwa kufanya
kazi kwa bidii kila mmoja na nafasi yake mahali alipo,na kwa wafugaji wafuge
kwa wingi pamoja na wakulima nao walime kwa bidii ili kuwa na ziada ya chakula
hapo ndipo tuataitendea haki kauli hiyo
‘’’’’’’Lengo
la kijiwe hiki na kauli yake ni kuunga mkono juhudi za mh.Rais kwa kazi
anazofanya.Tutumienafasi hii kuona namna ya kujikwamua kiuchumi ili kitongoji
cha mahove kipige hatua kimaendeleo ,wakulima mlime na wafugaji mfuge kwa
kuzingatia kanuni na taratibu za ufugaji kwa kfanya hivyo tutakuwa tumeitendea
haki kauli ya hapa kazi tu’’’’alisema
Baada ya
uzinduzi wa shina la wakeleketwa ulifanyika mkutano wa hadhara ambapo wananchi
walitoa kero zao kuhusiana na chanagamoto zinazowakabili ambazo hazijatatuliwa
kwa muda mrefu hadi sasa na hatiamae kutojua muafaka wa hitaji lao
Mzee Klelu Mahiteni alisema kuwa kutokana na uwingi
wao pamoja na vigezo vilivypo waliiomba serikali kuwapatia kijiji
ili waweze kupata huduma kama wananchi wengine lakini jambo la
kushangaza hadi hivi sasa hakuna kinachoendelea ukizingatia katika kampeni za
uchaguzi mkuu 2015 aliyekuwa mgombea wa ubunge kupitia chama cha mapinduzi
mh.Willium Lukuvi ambae ni waziri wa ardhi na makazi na mbunge wa jimbo hilo aliwaahidi
kuwa endapo atapewa dhamana ya ubunge atatoa upendeleo wa kupewa kijiji .
Tulikaa na
uongozi wa serikali za mitaa tukaandika barua ya kukumbusha ombi letu la kupewa
kijijiu lakini inashangazwa kuona barua hiyo haifanyiwi kazi wala kurudisha
majibu kama imekubalika au kukataliwa,tunaomba mh.mbunge wetu atusaidie kwa
kusimamia kama alivyoahidi kipindi cha kampeni ya uchaguzi mkuu wakati akiomba
kura’’’’alisema
Wakizungumza
katika mkutano huo wananchi walisema changamoto nyingine zinazowakabili
nipamoja na kivuko, darasa la chekechea ili watoto waweze kusoma maeneo jirani
na makazi yao,Zahanati ,bati kwa ajili ya kuezeka nyumba ya mchungaji wa kanisa
la kkt ambazo mh.Mbunge Lukuvi aliahidi kutoa.
Alisema
anaiomba serikali iweze kuwafikilia ili waweze kuepukanan na adha ya kushindwa
kuendelea na shughuli zao,kutokana na mvua kunyesha hasa katika kupata
matibabu pamoja na watoto kushindwa
kwenda shule kutokana na maji kujaa wakati wa masika.
Tatizo hili
limedumu kwa muda mrefu,na serikali inajua hilo lakini tunaona wapo kimya tu
bila kulifanyia kazi .Mvua zikianza kunyesha hali ya usalama inakuwa hatiani na
watoto wanashindwa kwenda shule pamoja ’’’alisema
Alisema serikali
inatakiwa kusimamia kuweka mgogolo baina ya wakulima na wafugaji na
kuweka utaratibu ambao utasaidia makundi haya yasiingilianae na kusababisha mtafaruku utakao vuruga amani
katika jamii miongoni mwao kutokana na wafugaji kupitisha mifugo yao katika vyanzo vya maji,na
mashambani na hatimae kusababisha maji kukauka.
0 maoni:
Chapisha Maoni