Na Mwandishi Wetu, Mwanza
Jumla
ya watoto 55 wamefanyiwa upasuaji katika kambi ya tiba ya watoto wenye
kichwa kikubwa na mgongo wazi, iliyowekwa katika hospitali ya Bugando
jijini Mwanza siku nne mfululizo, kufuatia tatizo la kichwa kikubwa
walilozaliwa nalo, chini ya udhamini wa taasisi ya GSM Foundation.
Zoezi litakalofanyika katika mikoa mitano ikiwa ni awamu ya kwanza kati
ya nne zinazotarajiwa kufanyika Tanzania nzima.
Akiongea
wakati wa kufunga kambi hiyo rasmi jioni ya leo, Daktari Bingwa wa
upasuaji na mifupa kutoka Taasisi ya Mifupa MOI, Dk Othman
Kiloloma(Pichani Juu) ambaye pia ni mratibu wa kambi hiyo aliishukuru
taasisi ya GSM kwa kuamua kulichukua tatizo hilo ambalo ameliita kuwa ni
kubwa ukilinganisha na jinsi linavyochukuliwa na jamii ya watanzania.
Dk
Kiloloma aliwaambia wanahabari kwamba jumla ya watoto 2000 huzaliwa na
vichwa vikubwa katika kanda ya Ziwa peke yake, na mtaalamu wa kuhudumia
wagonjwa wa namna hii ni mmoja tu ambapo pia kwa Tanzania nzima,
wataalamu wa upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa wako tisa tu.
Cha
kusikitisha ni kwamba kati ya hao, ni wachache sana hurudi kwa ajili ya
matibabu bali wengi wao hufariki kwa kufichwa ndani na wazazi wao aidha
kwa imani za kishirikina ama kushindwa kwa wazazi kumudu gharama za
matibabu.
Mpaka
jioni ya leo, ambayo ni siku ya nne tangu kuanza kwa kambi hii, jumla
ya watoto 55 walikuwa wameshafanyiwa upasuaji, ambapo siku ya kwanza,
walifanyiwa watoto 16, siku ya pili wakafanyiwa watoto 17, siku ya tatu
wakafanyiwa watoto 12, na leo wamefanyiwa watoto 10.
Mratibu
huyo ambaye pia ni Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji
(MOI), Dk Othman Kiloloma, amebainisha kwamba changamoto kubwa
inayotokea kwa jamii linapokuja suala la watoto wenye vichwa vukubwa na
mgongo wazi ni gharama za upasuaji, ambapo gharama ya upasuaji kwa mtoto
mmoja ni kati ya shilingi laki saba za kitanzania mpaka Milioni moja.
“Watoto
wengi huzaliwa katika mazingira duni na wazazi wasiokuwa na nguvu ya
kiuchumi, hali inayosababisha wengi wao kuwaficha ndani huku
wakiwahusisha na imani za kishirikina”, alifafanua Dk Kiloloma.
Dk
Kiloloma amesema zaidi ya watoto 4000 huzaliwa kila mwaka wakiwa na
tatizo la kichwa kikubwa, lakini wanaorudi Hospitali kwa ajili ya tiba
nhawazidi laki nne, swali kubwa ambalo jamii hujiuliza ni kuhusiana na
watoto ambao hawafiki hospitalini huishia wapi?
Kwa
upande wake, Halfan Kiwamba, Afisa Mawasiliano wa Taasisi ya GSM
Foundation ambao ndio washamini wakuu wa kambi hizo amesema, taasisi
yake imeamua kuokoa maisha y watoto hao ambao ni nguvukazi ya taifa la
kesho na inalifanya hilo ikiwa ni moja ya mikakati yake katika kurudisha
fadhila kwa jamii ya kitanzania ambao ni wateja wakubwa wa bidhaa za
GSM.
Kiwamba
amesema taasisi yake ina lengo la kuhakikisha kwamba wananchi wa
Tanzania hasa watoto ambao ni wa taifa ya kesho wanao msingi wa nguvu
kazi kwa ajili ya maisha yao ambapo vitu vikubwa ni elimu boira pamoja
na Afya.
Kwa
upande wake Meneja wa Taasisi ya GSM Shannon Kiwamba amesema wakati
mwingine ni vigumu kuingia katika maisha ya kila mwananchi na kumsaidia
mahitaji yake, lakini akiwa na uhakika wa Afya na elimu anaweza kwenda
mbali akijumlisha na jitihada zake.
Hivyo amewaomba watanzania kujitokeza wanaposikia taasisi yake inatoa huduma ili kufaidika nayo.
Kambi ya tiba ya GSM inaondoka kesho juijini Mwanza kuelekea Shinyanga ambapo itaweka kambi kwa siku tatu.
0 maoni:
Chapisha Maoni