Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Raisi Muungano za Mazingira Mhe. Luhaga Mpina ameshiriki usafi wa
mazingira wa kila jumamosi ya mwisho wa mwezi, mara hii mkoani Simiyu
katika wilaya ya Meatu jimboni Kisesa.
Akizungumza na wananchi wa eneo
la Mwandoya wilayani Meatu, Mhe. Mpina amewaasa wananchi wa mkoa wa
Simiyu kwa ujumla kuitunza miti 4820 iliyopokelewa na kupandwa
wilayani hapo baada ya serikali ya awamu ya tano kutekeleza ahadi yake
ya kuupatia Mkoa wa Simiyu idadi hiyo ya miti.
Naibu Waziri Mpina, alisema kuwa
kwa kuwamkoa wa simiyu huko kwenye hatari kubwa ya kuwa janga na umesha
wahi kukabiliwa na tatizo la uhaba wa chakula, kabla ya uchaguzi
uliopita, kwa kuitunza miti hiyo ya matunda wakazi wa mkoa huo
watanufaika na miti ya matunda hayo ya muda mfupi kwa kufanya biashara
ili kuweza kukuza uchumi na kuongeza kipato cha kila mmoja.
Aliongeza kuwa, zoezi la upandaji miti mkoani simiyu katika ma shule,
maeneo ya makazi ya watu na mashamba yanahitaji utunzani mkubwa kwani
miti hiyo ina uwezo mkubwa wa kuboresha uoto wa asili ambao mpaka hivi
sasa umetoweka.
Aidha Mhe. Mpina amewataka
viongozi wa mkoa wa Simiyu kuchukua nafasi yao kusimamia wanachi wafanye
usafi ikiwa ni agizo la serikali la kila mwisho wa mwezi kuwa siku ya
usafi na kuwa viongozi ambao watakuwa wazembe katika suala zima la
usimamiaji wa usafi wa mazingira watachukuliwa hatua.
Alipoongea na wanachi wa Jimbo La
Kisesa, Naibu Waziri Mpina aliwaasa wananchi wa Kisesa wa sapoti
jitihada za serikali za kupanda miti na kutunza mazingira, na kuwa
hakikishia wapiga kura wake kuwa pamoja na kuwa Naibu Waziri Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, nafasi za kazi yake kama Mbunge wa
jimbo hilo ipo pale pale na ataendelea kuwapigania wana Kisesa.
Aliwaomba wana Kisesa wawe mfano
wa kupanda miti iliyotolewa na serikali na kuitunza na kwa aliokosa
miche ya miti hiyo iliyogawiwa ame ahidi kuwapatia miche mingine kwani
shabaya yake kubwa ni kuwezesha mkoa wa simiyu kupata miti hasa ya
matunza na mbao ili kuboresha uchumi binafsi na pato la taifa.
Mhe. Mpina Amefanya usafi wa
mazingira leo katika eneo la hospital ya Mwandoya pamoja na kupanda miti
ikiwa ni sehemu ya utekekezaji wa kampeni ya kitaifa ya kupanda miti.
0 maoni:
Chapisha Maoni