Posted by Esta Malibiche on Nov3,2016 in NEWS
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe
Miraji Jumanne Mtaturu aliyesimama akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi
wa Mradi wa kuijengea jamii uwezo katika kuibua na kutekeleza mpango
shirikishi
Madiwani, na Wakuu wa Idara na
Vitengo wakisikiliza kwa makini maelezo kuhusu walengwa wa Mradi wa
kuijengea jamii uwezo katika kuibua na kutekeleza mpango shirikishi
Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya
Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya
ya Ikungi Ally Juma Mwanga, na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya
Wilaya ya Ikungi Bi Rustika Turuka
Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisikiliza kwa makini maelezo kuhusu mradi huo
Madiwani,Wakuu
wa Idara na Vitengo wakisikiliza kwa makini maelezo ya Mradi wa
kuijengea jamii uwezo katika kuibua na kutekeleza mpango shirikishi
………………………………………………….
Na Mathias Canal, Singida
Shirika la Health Actions
Promotion Association (HAPA) la Mkoani Singida kwa ushirikiano na
Shirika la The Foundation For Civil Society la Jijini Dar es salaam
linatarajia kuendesha mradi wa miaka mitatu kwa vijiji vyote vya Wilaya
ya Ikungi kwa lengo la kuijengea jamii uwezo na mbinu shirikishi kama
fursa na vikwazo katika maendeleo.
Mradi huo utaanza na Vijiji 10
vya majaribio (Pilot Villages) kutoka katika kata nne na kila kata
itakuwa na Vijiji ama viwili ama Vitatu ambapo uchaguzi wa Vijiji hivyo
vya majaribio umezuingatia utayari wa jamii husika katika shughuli za
maendeleo pamoja na gharama za uendeshaji wa mradi ili kupata matokeo
chanya kwa uendelezaji wa mradi husika.
Akizungumza wakati wa uzinduzi
huo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amesema kuwa
Uongozi wa Wilaya hiyo unaendelea kushirikisha wadau mbalimbali katika
kusaidia kutekeleza shughuli za maendeleo, kwani kwa uhabarisho wa
mafunzo ya kujenga uwezo wa jamii na Halmashauri yataendelea katika
kuimarisha juhudi za Wilaya zinazoendelea kuchukuliwa katika kutekeleza
miradi ya maendeleo pia itakuwa ni fursa kwa jamii kuwa na Uwezo na
Nyenzo muhimu katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa ufanisi.
Amesema kuwa Wilaya ya Ikungi
inakabiliwa na changamoto mbalimbali za kujiletea maendeleo ambapo
endapo zitapatiwa upembuzi yakinifu zitapunguza kadhia zinazowakumba
wananchi ambapo amezitaja changamoto hizo ikiwa ni pamoja na Ujenzi wa
Vituo vya Afya na Zahanati (Kata na Vijiji) ambapo kwa sasa Wilaya ina
vituo 39 tu vya kutolea huduma za Afya ambapo upungufu ni Asilimia 60,
Ujenzi na Uboreshaji wa miundombinu ya shule za msingi ambapo kuna
nyumba za walimu 387 ambapo upungufu ni nyumba 854, Ujenzi na Uboreshaji
wa majosho na mifugo kwani kwa sasa yapo majosho 30 huku kati ya hayo
majosho 20 ni mabovu.
Dc Mtaturu alisema kuwa Zipo
Asasi mbalimbali ambazo zimesajiliwa kwa lengo la kutoa elimu kwa
wananchi lakini zimegeuka na kuwa Asasi zinazofanya kazi za kisiasa
tofauti na usajili wao ambapo amesema serikali haitasita kuzichukulia
hatua ikiwemo kuzifuta Asasi hizo ili ziache kupotosha wananchi.
Dc Mtaturu alisema kuwa Mradi
huo unaotolewa na Shirika la HAPA ni lazima uzingatie matakwa ya kutoa
elimu kwa wananchi ili wafahamu kuwa wana nafasi kubwa ya kufanikisha
maendeleo yao katika jamii hivyo waache kupotoshwa na baadhi ya
wanasiasa kuwa maendeleo yataletwa na serikali pekee.
Msimamizi wa Mradi wa HAPA Noel
Makyao amewataja walengwa wa Mradi huo kuwa ni wananchi wote wa kijiji
cha Mradi wa majaribio, Wawakilishi 100 kutoka kila kijiji ambao
watachaguliwa ili kuendesha zoezi la kutengeneza bajeti ya mpango wa
kila mradi ulioibuliwa na jamii kwa siku tatu mfululizo na watu
mashuhuri, wakuu wa madhehebu ya dini na makundi mengine wapatao 20.
Alisema kuwa Jumla ya gharama
zote za kutekeleza mradi wa mbinu shirikishi ya kujenga uwezo wa jamii
katika kuibua, Kupanga, Kutekeleza na kupima matokeo ya Mradi katika
vijiji kumi vya majaribio kwa robo mbili zitakuwa shilingi milioni
hamsini (50,000,000/=).
Makyao alisema katika awamu hii
ya vijiji kumi vya majaribio jumla ya watu wapatao 25,511 watafikiwa
kati ya lengo la watu 25,334 zaidi ya watu 177 ya walengwa wa mradi.
0 maoni:
Chapisha Maoni