Shirika la Umoja wa
Mataifa limenyakua tuzo ya mwoneshaji bora kwenye kategori ya habari,
machapisho, uchapishaji na vifaa vya ofisini katika sherehe za uzinduzi
wa maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye kwenye
viwanja vya Mwalimu Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Tuzo hiyo imekabidhiwa na mgeni
rasmi Rais wa Rwanda Mh. Paul Kagame na kupokelewa na Mkuu wa Masharika
ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Bw.
Alvaro Rodriguez.
Umoja wa Mataifa umekuwa kinara
wa kuelimisha wananchi, kupitia njia mbalimbali ikiwemo redio, magazeti
mitandao ya kijamii na pia kushiriki katika maonyesho ya sabasaba kila
mwaka kwa Zaidi ya miaka 6 na kwa miaka 5 mfululizo wamekuwa wakishinda
tuzo hizo.
Umoja wa Mataifa mwaka huu
umekuja na kampeni ya uhamasishaji wa Malengo ya dunia (Global Goals) na
umuhimu wa watanzania kuyaelewa malengo hayo na kuwa mabalozi katika
kuhakikisha malengo hayo mapya ya maendeleo endelevu (SDGs)
yanatekelezeka.
Banda la Umoja wa Mataifa
linapatikana katika ukumbi wa Karume yanakoendelea maonyesho ya 40 ya
Biashara ya Kimataifa almaarufu ‘sabasaba’ katika viwanja vya Mwalimu
Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Rais wa Rwanda Paul Kagame, (wa
pili kulia) akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dk. John Pombe Magufuli, (wa kwanza kulia), akimkabidhi tuzo ya
mwoneshaji bora kwenye kategori ya habari, machapisho, uchapishaji na
vifaa vya ofisini, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Bw. Alvaro Rodriguez, wakati
wa uzinduzi wa maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam
kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Julai 1, 2016.
Wapili kushoto ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mh. Charles
Mwijage.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Bw.
Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na wafanyakazi
wa Umoja wa Mataifa wakiwa na tuzo ya ushindi katika banda lao. Kulia
Felister Bwana wa Shirika la UNFPA Tanzania, Didi Nafisa (wa pili kulia)
pamoja na Hoyce Temu (kushoto).
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Bw.
Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na wafanyakazi
wa Umoja wa Mataifa wakiwa na tuzo ya mwoneshaji bora kwenye kipengele
cha habari, machapisho, uchapishaji na vifaa vya ofisini katika banda
lao. Kulia Felister Bwana wa Shirika la UNFPA Tanzania, Didi Nafisa (wa
pili kulia), Hoyce Temu (katikati) pamoja na Edgar Kiliba (kushoto).
Wataalamu wa mawasiliano na
Uhamasishajii (Communications, Advocacy and Partnership-COAP) wa ofisi
ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini wakifurahia
ushindi huo katika banda lao. Kutoka kushoto ni Edgar Kiliba, Hoyce Temu
na Didi Nafisa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Bw.
Alvaro Rodriguez (kulia) katika picha ya pamoja na vijana wanaojifunza
kazi ‘Intern’ katika ofisi za Umoja wa Mataifa, Edgar Kiliba (katikati)
na Msafiri Manongi.
Wananchi wakisaini kitabu cha
wageni katika banda la Umoja wa Mataifa lililopo ukumbi wa Karume kwenye
Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa almaarufu Sabasaba katika
viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa jijni Dar es Salaam.
Kijana Msafiri Manongi
anayejifunza kazi ‘Intern’ (kushoto) wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji
(IOM), akitoa maelezo ya kazi mbalimbali zinazofanywa na mashirika ya
Umoja wa Mataifa nchini sambamba na elimu ya Malengo ya Dunia (Global
Goals) kwa Maendeleo Endelevu kwa kijana mwenzake (jina halikuweza
kupatikana) aliyetembelea banda UN kwenye maonyesho ya Sabasaba
yanaoendelea kutimua vumbi jijini Dar es Salaam.
Kijana Msafiri Manongi
anayejifunza kazi ‘Intern’ kwenye Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM)
(kushoto) akipozi na kijana mwenzake aliyetembelea banda la UN
kujifunza shughuli mbalimbali za UN Tanzania na kujinyakulia zawadi ya
tisheti.
Kijana Edgar Kiliba
anayejifunza kazi ‘Intern’ katika kitengo cha Mawasiliano katika Ofisi
ya Mkuu wa Umoja wa Mataifa Tanzania (kulia), akitoa elimu ya Malengo ya
Dunia (Global Goals) kwa Maendeleo Endelevu kwa wananchi wanaoendelea
kufurika kwenye banda la Umoja wa Mataifa katika maonyesho ya Sabasaba
yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Ofisa wa Mawasiliano na
Ushirikiano NUNV kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa, Didi Nafisa akitoa maelezo ya kazi mbalimbali za Umoja wa
Mataifa kwa Bw. Rehani Athumani wa NHIF (kulia) aliyetembelea banda la
UN Tanzania katika maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja
vya Mwalimu Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Katikati ni
Kijana Edgar Kiliba anayejifunza kazi ‘Intern’ katika kitengo cha
Mawasiliano katika Ofisi ya Mkuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa
Tanzania.
Makamu wa Rais wa Powerline
Technologies Limited, Bw. Tumu Kaisi (kushoto) akibadilishana uzoefu na
Kijana Msafiri Manongi anayejifunza kazi ‘Intern’ (kushoto) wa Shirika
la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) alipotembelea banda la Umoja wa Mataifa
kwenye maonyesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Ofisa wa Mawasiliano na
Ushirikiano NUNV kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa, Didi Nafisa akimbandika zawadi ya beji ya’ HE 4 SHE’ ya Shirika
la UN Women katika kampeni ya kuhamasisha wanaume waweze kuwasapoti
wanawake katika nyanja mbalimbali kwa mmoja wa wananchi wanaoendelea
kutembelea banda la Umoja wa Mataifa katika maonyesho ya Sabasaba
yanayoendelea kushika kasi jijini Dar es Salaam.
Pichani juu na chini ni Baadhi
ya wananchi wakisoma vipeperushi na majirada mbalimbali katika banda la
Umoja wa Mataifa lililopo katika ukumbi wa Karume kwenye maonyesho ya
Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Mtoto akisoma moja ya vitabu
vyenye michoro ya katuni ambacho kilimvutia akisome alipotembelea banda
la Umoja wa Mataifa na wazazi wake.
Mmoja wa wananchi aliyetembelea
banda la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya Sabasaba akifurahia
zawadi ya tisheti yenye ujumbe mzito wa kukomesha ukatili wa kijinsia
inayosomeka “FUNGUKA” Tumia malaka yako KUZUIA UKATILI WA KIJINSIA.
Kulia ni Ofisa wa Mawasiliano na Ushirikiano NUNV kutoka Ofisi ya
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Didi Nafisa.
Mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni
ya Zaidi Enterprises, Eng. Allen Kimambo katika picha na mabango ya
Malengo ya Dunia (Global Goals) ambayo ni sehemu anayoyafanyia katika
utekelezaji wa kuhakikisha malengo hayo yanafanikiwa.
Mtaalamu wa Mawasiliano
Mwandamizi wa Ukanda wa Afrika wa Jhpiego, Bw. Charles Wanga akiwa na
mabango ya Malengo ya Dunia (Global Goals) kwa Maendeleo Endelevu katika
banda la UN Tanzania.
Mkutubi wa kituo cha Habari cha
Umoja wa Mataifa (UNIC), Harriet Macha katika picha ya pamoja na mmoja
wa vijana aliyetembelea banda la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya
Sabasaba.
Watoto nao waliwakilisha
Malengo ya Dunia kwa Maendeleo Endelevu. Kulia ni Msafiri Manongi kutoka
Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM).
Vijana wanaojifunza kazi katika
Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini ‘Intern’ Edgar Kiliba (kushoto) na
Msafiri Manongi (kulia) katika picha ya pamoja na wananchi
wanaotembelea banda la Umoja wa Mataifa kujifunza shughuli mbalimbali
zinazofanywa na Mashirika hayo nchini.
0 maoni:
Chapisha Maoni