Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akizungumza na timu ya mpira wa miguu ya wasichana ya umri wa miaka 11 Fc Vito Malaika na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hafla ya kukabidhi Bendera ya Taifa kwa timu hiyo kwenda kushiriki mashindano ya mpira wa miguu ya Helsinki Cup nchini Finland Julai 8 mwaka huu kushoto Mwakilishi wa Sport Development Aid Bw. Chigogolo Mohamed.
Naibu
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe Annastazia James
Wambura (wa pili kulia) akikabidhi Bendera ya Taifa kwa nahodha timu ya
mpira wa miguu Fc Vito Malaika Alia Fikiri (kushoto) kwenda kushiriki
mashindano ya Helsinki Cup nchini Finland Julai 8 mwaka huu.
( Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM)
———————————–
Na Raymond Mushumbusi WHUSM
Serikali imeazimia kujenga na
kuendeleza shule za michezo zilizopo katika mikoa yote nchini kwa
kipindi hiki cha Serikali awamu ya tano.
Azimio hilo limetolewa leo Jijini
Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.
Annastazia James Wambura wakati akizungumza na timu ya mpira ya miguu ya
wasichana ya Fc Vito Malaika katika hafla ya kukabidhi Bendera ya Taifa
kwa timu hiyo kwenda kushiriki mashindano ya mpira wa miguu ya Helsinki
Cup yatakayofanyika nchini Finland Julai 8 mwaka huu.
“Azima ya Serikali ya Awamu ya
Tano ni kuendeleza michezo nchini kwa kuibua vipaji vya michezo na
kuviendeleza kuanzia wakiwa shule” Alisema Mhe. Annastazia.
Mhe Annastazia Wambura ameongeza
kuwa Serikali ya Tanzania inashirikia na Serikali ya Finland katika
kuendeleza michezo shuleni na zaidi ya shule 462 nchini zitafaidika na
miradi ya michezo ya vijana inayofadhiliwa na Serikali ya Finland.
Kwa upande wake Balozi wa Finland
nchini Tanzania Pekka Hukka amesema kuwa wamedhamiria kushirikiana na
Serikali ya Tanzania katika kuendeleza michezo nchini hasa kwa vijana
ili kujenga timu nzuri za baadae, na kwa sasa wanapeleka timu za vijana
kwenda kushiriki mashindano mbalimbali ya kimataifa ikwemo Helsinki Cup
linalofanyika nchini finland Julai 8 mwaka huu.
Naye Meneja wa Timu ya wasichana
ya mpira wa miguu ya Fc Vito Malaika Bakari selemani ameipongeza
Serikali kwa juhudi zake za kuendeleza michezo hasa kwa vijana kwa
kushirikiana na Taasisi mbalimbali na ili kuendeleza michezo na kukuza
vipaji kwa vijana Serikali na wadau wa michezo wametakiwa kuwekeza kwa
vijana ili kujenga timu zenye kuleta ushindani katika mashindano ya
kitaifa na kimataifa.






0 maoni:
Chapisha Maoni