Jumatatu, 4 Julai 2016
PICHA: Satelite ya Juno yaifikia obiti ya sayari ya Jupita
22:20
No comments
Safari
ya miaka mitano ambayo imefanywa na satelite ya Juno iliyotengenezwa na
wanasayansi wa nchini Marekani imekaribia kukamilika kwa satelite hiyo
kutua katika sayari kubwa kuliko zote ya Jupita.
Satelite
ya Juno imefika katika obiti ya Sayari ya Jupita na baada ya kutua
inataraji kudumu katika sayari hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu
ili kufanya uchunguzi kuhusu uumbwaji wa sayari ya Jupita na mazingirra
yake jinsi yalivyo.
Awali kabla ya kufika katika obiti ya sateliye hiyo, wanasayansi nchini
Marekani ambao wapo katika moja ya maabara ya kisayansi katika Chuo cha
Teknolojia cha California walionekana kuwa watulivu na wakisubiri kwa
makini kuona jinsi chombo hicho kitakavyofika katika obiti na baada ya
kupokea ripoti ya sauti kutoka katika satelite ya Juno iliyosema “Karibu
Jupita, Roger Juno” walionekana kushangilia kwa furaha kwa kufanikisha
jambo walilotamani kutokea kwa muda mrefu.
Mmoja
wa wanasayansi alipokuwa akizungumza kabla ya kutua kwa chombo hicho
alisema kwa kipindi cha miaka mitano wamekuwa hawa hawapumziki kwa muda
wa kutosha kutokana na kila muda kutaka kuangalia hali ya Juno kama ipo
salama katika safari yake kuelekea sayari ya Jupita.
Wanasayansi Marekani wakisubiri kwa hamu kuona satelite ya Juno ikifikia obiti ya Jupita.
Satelite ya uno ikiwa ilipokuwa njiani kuifikia obiti ya Jupita.
Wanasayansi wakipongezana baada ya Juno kuifikia obiti ya Jupita.






0 maoni:
Chapisha Maoni