……………………………………………………………………………………………
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Mhe. Paul Makonda amewataka Wakuu wapya wa Wilaya kuimarisha ulinzi na
usalama kwa wananchi waliopo katika Wilaya zao ili kudumisha amani.
Makonda alisema hayo leo jijini
Dar es Salaam wakati akizungumza na Wakuu wa Wilaya juu ya kuwalinda
wananchi na mali zao na kuhakikisha usalama unakuwepo katika Wilaya
wanazozisimamia.
Alieleza kuwa kwa kuwa wao ndio
wanaomuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli katika Wilaya zao, wanatakiwa kuhakikisha wametekeleza
ahadi zilizotolewa na Mhe. Rais wakati wa kampeni.
“Ningependa wakuu wangu wa Wilaya
mchukiwe kwa kusimamia Haki na Sheria kuliko kukumbatia uovu kwa
kuhitaji furaha ya muda mfupi, hakikisheni Sheria na Kanuni zilizopo
kwenye Katiba ndio ziwe muongozo wenu”, alisema Makonda.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es
Salaam aliwataka Wakuu wa Wilaya zake kuwasimamia Wakurugenzi wao ili
kuhakikisha wanatumia bajeti waliyopewa katika kutatua changamoto
zilizopo katika Wilaya zao.
Aidha, Makonda amewasisitiza
kuhakikisha kuwa kuanzia Julai 11 mwaka huu maeneo yote yanayofanya
biashara ya shisha kufungwa na kuweka maeneo maalumu kwa ajili ya
kuvutia sigara.
Wakuu wa Wilaya wapya wamepewa
wiki mbili za kutengeneza mpango kazi kwa kusoma ilani ya Chama cha
Mapinduzi (CCM), Hotuba ya Mhe.Rais John Magufuli aliyoisoma wakati wa
ufunguzi wa Bunge la 11 la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na mazingira
ya kazi katika maeneo yao.
0 maoni:
Chapisha Maoni