Saudia
inatarajiwa kuwapatia bangili za kielektroniki mahujaji wanaoelekea
Mecca kwa Hajj ya mwaka huu ambalo ni kongomano kubwa la Waislamu kutoka
kote duniani.
Hatua
hiyo inafuatia mkanyagano uliotokea mwaka uliopita ambapo zaidi ya
mahujaji 750 wanaaminikia kuuawa huku wengine 900 wakijeruhiwa.
Bangili
hizo zitakuwa na habari za kibinafsi za kila hujaji pamoja na zile za
matibabu kusaidia mamlaka ya Saudia kuwatambua na kuwalinda mahujaji
hao.
Takriban kamera 1000 pia zimewekwa.
Bangili
hiyo ya utambulisho itukuwa na habari muhimu kama vile pasipoti na
anwani lakini pia zitatoa habari kwa mahujaji kama vile mda wa ibada
pamoja na lugha tofauti kuwasaidia wale wasiozungumza lugha ya Kiarabu
wakati huo.
Bangili hizo zitakuwa haziingii maji na zitaunganishwa na programu ya ramani.
0 maoni:
Chapisha Maoni