KAMPUNI
ya Kitanzania ya Afri Tea and Blrenders (1963) Ltd, inayozalisha bidhaa
bora zinazotangaza vivutio mbalimbali na Uchumi wa Tanzania kama Majani
ya Chai ya Green Label, African Pride Tea, Kilimanjaro Infusions, Simba
Chai, Kahawa ya Africafe na Uji Bora, wameibuka kidedea katika Maonesho
ya Biashara ya Kimataifa kwa kunyakua Tuzo ya Mshindi wa Kwanza wa
Maonesho ya Bidhaa Bora za Vyakula na Vinywaji 2016.
Akizungumza
na Mtandao huu Mkuu wa Idara ya Masoko, Biashara ya Nje na Wateja, Bw.
Zachy Irenus Mbena, alisema kuwa hii ni Tuzo ya tatu kwa mwaka wa tatu
mfululizo kupata ambapo mwaka 2014 wapitwaa Tuzo ya mshindi wa kwanza,
2015 walipata Tuzo ya mshindi wa pili ya Wauzaji wa Bidhaa za Tanzania
Nje ya Nchi (Best Exporting) na mwaka huu wamerejea katika nafasi ya
kwanza.
Aidha
Mbena alisema kuwa anawashukuru waeteja na watumiaji wa bidhaa zao
waliowafanya kuweza kutambulika Kimataifa kwa kutangaza Uchumi, Vivutio
na Utalii wa Tanzania kupitia bidhaa zao kama Mlima Kilimanjaro,
Wanyama, Khanga Vazi la asili ya Kimasai na Utamaduni wa Mtanzania kwa
ujumla.
Kampuni
hiyo imezidi kujizolea sifaa kabambe kwa kuwa wabunifu katika kuzalisha
Bidhaa zinazoendana na mahitaji halisi ya Watanzania.
Rais
wa Rwanda Paul Kagame, (wa pili kulia) akimkabidhi Mkuu wa Idara ya
Masoko, Biashara ya Nje na Wateja, Bw. Zachy Irenus Mbena, Tuzo ya
Mshindi wa Kwanza wa Maonesho ya Bidhaa Bora za Vyakula na Vinywaji
2016, wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa kwenye
Viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba Julai 2, 2016.
Aidha Kampuni hiyo imezalisha
bidhaa pekee inayotangaza Kisiwa cha Zanzibar ‘Africafe Zanzibar Spice
Coffee’ iliyochanganywa na Karafuu huku ikiwa katika muonekano wa
kuvutia inajitangaza kimataifa, iliyohifadhiwa katika Kasha
lililonakshiwa ramani ya Kisiwa cha Zanzibar na baadhi ya alama za
Kisiwa hicho.
‘’Pamoja na hayo lakini pia tunashiriki katika maonesho mbalimbali ya Nje ya nchi yanayoandaliwa na Mabalozi wetu wa Tanzania nchi za Nje ‘Tanzania Day in Embasses’ ambapo mwezi uliopita tulialikwa kushiriki maonesho yaliyofanyika katika jiji la Antalya Uturuki, ambayo pia yalishafanyika Msumbiji, Uingereza, Ethiopia na Rusia’’.
Alisema Mbena Pia wamekuwa wakushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Maendeleo ya Biashara Tanzania ‘TAN TRADE’ katika maonesho mbalimbali ya Kimataifa.
Kutokana na umuhimu na ubora wa bidhaa zao zinazotengenezwa kiasili, wamekuwa wakishiriki pia katika maonesho mbalimbali ya Sikukuu ya Wakulima Nane Nane katika Mikoa ya Mbeya, Arusha na Morogoro.

Muonekano wa Banda la Maonesho la Afri Tea and Blenders (1963) Ltd.
Aidha Bw. Mbene aliwakaribisha Wanzania wote wanaofika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere kutembelea Mabanda ya maonesho kufika katika Banda lao linalotoa huduma kufuturisha BURE kwa wafungaji mida ya jioni ambao hupewa fursa ya kuonja chai za aina zote pamoja na Chai, Uji, Kahawa na Maji bila malipo yeyote.
Pamoja na hayo pia wananchi wanaofika katika Banda hilo hupewa zawadi ya Pakiti moja Majani ya Chai yenye mchanganyiko wa radha tofauti tofauti za Green Tea, Hibiscus, Rooibos, Paper Minty, Camomile, Vanilla na Morocco Minty.
Imeandaliwa na Ripota wa Sufianimafoto, Dar

Afisa Masoko na Mauzo wa
Kampuni ya Afri Tea and Coffee (1963) Ltd, Sheila Manafi, akipozi na
Tuzo waliyokabidhiwa na Rais Kagame.
Baadhi ya Wananchi waliofika katika Banda hilo wakinunua na kuonja radha tofauti za Chai za Kampuni hiyo.
Muonekano wa Mandhari ya
banda hilo lililo katika maonesho hayo likiwa na baadhi ya vitu vyenye
muonekano wa Tamaduni za Kitanzania.
Baadhi ya Wananchi waliofika katika Banda hilo wakionja radha za Chai na Kahawa za Kampuni hiyo.
Mfanyakazi wa Kampuni hiyo, Cecilia Mrema (kulia) akitoa maelezo kwa baadhi ya wateja katika Banda hilo.
Mfanyakazi wa Kampuni hiyo, Ronne Zachy (kushoto) akifafanua jambo kwa baadhi ya wateja waliotembelea Banda hilo.
Sheila akipanga bidhaa…..
Baadhi ya wateja wakipata maelezo kutoka kwa wahudumu wa Kampuni hiyo.
Mfanyakazi wa Kampuni hiyo, Cecilia Mrema (kulia) akitoa maelezo kwa baadhi ya wateja katika Banda hilo.
Baadhi ya wananchi waliofika katika Banda hilo wakionja ladha tofauti za Chai na Kahawa za Kampuni hiyo.
Karibu katika banda la
maonesho la kampuni ya Afri Tea and Coffee Blenders 1963 Ltd katika
maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba 2016.
0 maoni:
Chapisha Maoni