Katibu Mkuu wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Tanzania (THERIA), Rehema Mwaipaja akizungumza na wanachama wa THERIA kabla ya kufungwa kwa Mkutano wao juzi. |
Katibu Mkuu wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Tanzania (THERIA), Rehema Mwaipaja akizungumza na wanachama wa THERIA kabla ya kufungwa kwa Mkutano wao juzi. |
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Bi. Ummy Mwalimu ameziagiza hospitali
mbalimbali nchini kuhakikisha zinachukua tahadhari za kuwalinda
wafanyakazi wake kitengo cha kumbukumbu katika mazingira ya kupata
maambukizi hasa wanapokuwa kazini wakitimiza majukumu yao.
Waziri, Mwalimu ametoa maagizo
hayo kupitia hotuba yake iliyosomwa na Mkurugenzi wa Uhakiki Ubora wa
Huduma za Afya kutoka wizara hiyo, Dk. Mohamed A. Mohamed
alipomwakilisha katika hafla ya kufungwa kwa mkutano wa Chama cha
Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Tanzania (THERIA) zilizofanyika
juzi jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika hafla hiyo, Dk.
Mohamed alisema wizara hiyo, inatambua mazingira hatarishi ambayo
wafanyakazi wa kitengo cha kumbukumbu wamekuwa wakifanyia kazi hasa
ukizingatia wao ndio watu wa kwanza kukutana na wagonjwa kabla ya kufika
kwa madaktari jambo ambalo linaweza kuzua maambukizi kwa magonjwa
yaambukizwao kwa njia ya hewa.
“..Natambua pia mazingira
mnayofanyia kazi wengi wenu yanayowafanya kuwa kwenye hatari ya kupata
magonjwa ya kuambukiza kwani nyie ndo wa kwanza kabisa kukutana na
mgonjwa, kabla ya kuonana na daktari au mtaalamu wa vipimo, hivyo kupata
maambukizi ya magonjwa hatarishi hasa yaambukizayo kwa njia ya hewa na
mengineyo ni rahisi. Woizara yangu inapenda kuwaagiza Wakuu wote wa
hospitali nchini kuhakikisha wanarekebisha mazingira mnayofanyia kazi
ili kuondoa hali hii,” alisema Dk. Mohamed akimwakilisha waziri wake.
Aidha wizara hiyo pia iliahidi
kushughulikia kero ya uhaba na ukosefu wa wafanyakazi wa taaluma ya
utunzaji kumbukumbu za afya kwenye vituo vya afya na hospitali hapa
nchini ikiwa ni pamoja na kuzitaka hospitali na vituo hivyo kuajiri watu
wenye taaluma halisi ya utunzaji kumbukumbu na kuhakikisha kada hiyo
inapata muundo, stahili zake na kutambulika kama ilivyo kwa makundi ya
kada nyingine.
Kwa upande wake Katibu wa Chama
cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Tanzania, Rehema Mwaipaja
akizungumza katika mkutano huo alisema kuwa THERIA ina umuhimu mkubwa
hasa ukizingatia kuwa takwimu sahihi za afya ndio msingi bora kwa huduma
kamilifu kwa jamii. Aliongeza kuwa uboreshaji wa hali ya ukusanyaji,
uchambuzi na utunzaji wa takwimu sahihi za afya unachangia kuboresha
tafiti mbalimbali za afya ambazo ni matunda ya ukuaji na uboreshaji wa
huduma kiujumla.
“Nidhahiri kuwa ukuaji wa taaluma
ya afya hutegemea sana tafiti mbalimbali zitokanazo na taarifa
zilizokusanywa na kutunzwa kikamilifu kazi ambayo ni ya msingi kwa afisa
kumbukumbu wa afya mahali popote anapofanya kazi, hayo yote huleta
faida kwa wagonjwa, taasisi na kwa wafanyakazi,” alisema Bi. Mwaipaja.
Wanachama wa THERIA kutoka mikoa
mbalimbali walikutana kwa siku mbili mfululizo katika wao mkuu
uliofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine mkutano
huo ulifanya uchaguzi kupata viongozi wapya wa chama hicho.
0 maoni:
Chapisha Maoni