Posted by Esta Malibiche on Oct 2,2016 in NEWS
Mkurugenzi wa Kurgenzi ya Mawasiliano wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Bernard James
……………………………………………………….
Na: Mwandishi Wetu.
MUSWADA wa huduma za Habari wa
mwaka 2016 umeelezewa kuwa muarubani wa uandishi wa habari za kughushi
na uchochezi kutokana na kuwa na vifungu vyenye kumlinda mwandishi na
kumuweka hatiani pindi anapoenda kinyume na matakwa ya sheria.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi
wa Kurgenzi ya Mawasiliano wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Bernard
James wakati wa mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii leo Jijini
Dar es Salaam.
“Baadhi ya waandishi wa habari
wamekuwa na tabia za kandika habari za kughushi na mara nyingine zenye
lengo la kumkashfu mtu, ni imani yangu kwamba muswada huu ni muafaka kwa
watu kama hao”. Alisema Bernard.
Bernard alivitaja vifungu hivyo
kuwa ni Sehemu ya Tano ya muswada huo kuanzia kifungu cha 32 hadi 39
ambavyo vinahusu mambo ya kashfa ambapo mwandishi ana anayo haki yake,
hali kadharika anao wajibu wa kuzingatia misingi ya sheria na mipaka
yake.
Huku sehemu ya saba ikihusisha
makosa mbalimbali yakiwemo uchochezi,habari za kuchochea uasi, makosa
yanayohusu utangazaji, vyombo vya habari na kosa la habari za kutia hofu
kwa jamii.
Alisema kuwa ni vyema wanahabari
wakatambua kwamba Serikali imeleta muswada huo si kwa nia ya kukandamiza
uhuru wa habari bali ni nia yake yakutaka kuona kunakuwa na maboresho
katika tasnia ya hii na siyo kama ambavyo wengi wao wamekuwa
wakipotosha.
Aidha Bernard aliongeza kuwa
muswada huo ukipitishwa utapelekea kuanzishwa kwa chombo
kitakachosimamia waandishi wa habari kwa kuwapa Vitambulisho, kusimamia
maadili na mienendo ya taaluma za waandishi wa habari na kuongeza kuwa
tasni itaheshimika kwani wale makanjanja hawatakuwa na nafasi tena.
“Binafsi naunga mkono muswada huu upitishwe ili tasnia ya habari iheshimike kama taaluma nyingine zinavyoheshimika”.Aliongeza.
Amewaomba wanahabari wenzake
kuunga mkono Muswada huu unaotarajiwa kusomwa Bungeni kwa mara ya pili
siku ya Ijumaa ya tarehe 4 Novemba ambapo utajadiliwa na kupitihwa.
0 maoni:
Chapisha Maoni