Katika kuhakikisha wahalifu hawapati nafasi ya kutamba
nchini, makamanda wa Polisi wa mikoa, wakuu wa upelelezi na waendesha
mashtaka wameazimia kuboresha ushirikiano wao katika kufanikisha kesi za
wahalifu pindi zinapofikishwa mahakamani ili waweze kupewa adhabu kali
kwa mujibu wa sheria.
Hayo yamo katika maazimio ya watendaji hao wa haki jinai
nchini katika kikao kazi cha siku mbili kilichofanyika mkoani Dodoma na
kuwashirikisha makamanda wa polisi wa mikoa, mawakili wafawidhi wa
mikoa na wakuu wa upelelezi wa mikoa.
Kikao hicho kilikuwa chini ya uenyekiti wake Mkuu wa Jeshi
la Polisi, IGP Ernest Mangu pia kilihudhuliwa na mkurugenzi wa Mashtaka
nchini, DPP Biswalo Mganga, Makamishina wa Polisi, pamoja na taasisi
mbalimbali zinazohusika na upelelezi na uendeshaji wa mashtaka.
Wapelelezi hao na waendesha mashtka walisema wataendeleza
program za mafunzo ya pamoja katika ngazi ya mkoa, kufanya vikao vya
mara kwa mara ili kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili na
kuendana na kasi ya Serikali ya awamu ya tano lengo likiwa kuharakisha
upelelezi na kutoa haki kwa watuhumiwa.
Aidha, wajumbe hao wa haki jinai wameazimia pia
kukabiliana na changamoto ya ucheleweshaji wa upelelezi wa kesi ambapo
wamekubaliana kwa pamoja kuzifikisha mahakamani kesi zote zenye ushahidi
wa moja kwa moja ili kuondokana na kesi kuchua muda mrefu na kuleta
malalamiko kwa wananchi.
0 maoni:
Chapisha Maoni