Mwenyekiti
wa Baraza la Vyama vya Siasa Nchini Mhe. Peter Kuga Mziray akifafanua
jambo wakati wa kikao cha Baraza kujadili Mapendekezo ya Mfumo wa
utatuzi wa migogoro ndani na baina ya vyama vya siasa kilichofanyika
mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa GEPF Victoria Jijini Dar es salaam .
Kulia ni Mhe. Jaji Francis S.K Mutungi, Msajili wa Vyama vya Siasa na
Mhe. Vuai Ali Vuai, Makamu Mwenyekiti wa Baraza .
Bw.
John Cheyo mmoja wa wajumbe wa Baraza la vyama vya siasa akichangia
hoja wakati wa kikao cha Baraza kujadili Mapendekezo ya Mfumo wa
utatuzi wa migogoro ndani na baina ya vyama vya siasa kilichofanyika
mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa GEPF Victoria Jijini Dar es salaam.
Baadhi
ya wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa wakifuatilia mjadala wakati wa
kikao cha Baraza kujadili Mapendekezo ya Mfumo wa utatuzi wa migogoro
ndani na baina ya vyama vya siasa kilichofanyika mwishoni mwa wiki
katika ukumbi wa GEPF Victoria Jijini Dar es salaam.
Baadhi
ya wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa wakifuatilia mjadala wakati wa
kikao cha Baraza kujadili Mapendekezo ya Mfumo wa utatuzi wa migogoro
ndani na baina ya vyama vya siasa kilichofanyika mwishoni mwa wiki
katika ukumbi wa GEPF Victoria Jijini Dar es salaam.
Baadhi
ya wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa wakifuatilia mjadala wakati wa
kikao cha Baraza kujadili Mapendekezo ya Mfumo wa utatuzi wa migogoro
ndani na baina ya vyama vya siasa kilichofanyika mwishoni mwa wiki
katika ukumbi wa GEPF Victoria Jijini Dar es salaam.
Picha
ya Pamoja ya Wajumbe wa Baraza la vyama vya Siasa baada ya kikao cha
Baraza kujadili Mapendekezo ya Mfumo wa utatuzi wa migogoro ndani na
baina ya vyama vya siasa kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi
wa GEPF Victoria Jijini Dar es salaam.
………………………………………………………………………………………………………
Na Monica Laurent -Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa
Wajumbe wa Baraza la Vyama vya
Siasa Nchini ambalo linaundwa na wawakilishi wawili kutoka kila chama
cha siasa chenye usajili wa kudumu wamekutana mwishoni mwa wiki katika
ukumbi wa mikutano wa GEPF uliopo Victoria Jijini Dar es salam kujadili
mapendekezo ya mfumo wa utatuzi wa migogoro ya ndani na baina ya vyama
vya siasa .
Mapendekezo hayo yalitolewa na
Mtaalamu wa utatuzi wa Migogoro Bw. Ghalib Galant ambaye awali alifanya
utafiti wa utatuzi wa migogoro ya ndani na baina ya vyama vya siasa
nchini chini ya usimamizi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na
kwa udhamini wa UNDP kupitia mradi wake wa “Democratic Project” ukiwa
na lengo la kuiboresha sura namba 258 ya Sheria ya Vyama vya Siasa ya
mwaka 1992 ili kuendana na mahitaji ya ukuaji wa demokrasia nchini.
Utafiti huo ulishirikisha wadau mbalimbali wa demokrasia ya vyama vingi
nchini vikiwemo vyama vya siasa.
Akiwasilisha mapendekezo, Msajili
Msaidizi Bi. Piencia C. Kiure ,alisema kuwa ilipendekezwa kuwa Sheria
ya Vyama vya Siasa nchini iweke masharti yanayohusu utaratibu wa
kutatua migogoro ndani na baina ya vyama vya siasa “ migogoro ndani ya
chama ni lazima ishughulikiwe kwanza ndani ya chama cha siasa na
kufikia tamati kwa mfumo wa utatuzi wa migogoro uliowekwa kwa mujibu wa
katiba ya chama, kabla ya kuwasilishwa katika Ofisi ya Msajili wa Vyama
vya Siasa kwa ajili ya upatanishi” ilikaririwa sehemu ya mapendekezo
“Upatanishi ukishindikana mgogoro
husika uwasilishwe kwenye Baraza la Uamuzi la Migogoro ya Vyama vya
Siasa kwa uamuzi. Ikiwa muhusika wa mgogoro asiporidhika na uamuzi wa
Baraza la Uamuzi wa migogoro ya vyama vya siasa atawasilisha mgogoro
husika Mahakama Kuu mbele ya Majaji watatu kwa mapitio ya uamuzi wa
Baraza. Muhusika asiporidhika na uamuzi wa Mahakama Kuu, atakata rufaa
Mahakama ya Rufaa” ilifafanua sehemu ya Mapendekezo.
Aidha kumekuwa na msisitizo wa
kufuata mtiririko wa hatua katika utatuzi wa migogoro kama
ilivyobainishwa hapo juu ili kuepusha migogoro ndani ya vyama kwenda
moja kwa moja Mahakamani ambako huchukua muda mrefu na kuathiri ukuaji
wa demockaria ndani na nje ya vyama vya siasa hapa nchini.
Wakichangia katika mjadala huo,
baadhi ya wajumbe walikubaliana na hoja kuwa vyama vya siasa vitatue
kwanza migogoro yake ndani ya vyama na kwamba pale tu itakaposhindikana
ndipo ipelekwe kwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.
Wajumbe walishindwa kukubaliana
katika hoja ya uwepo wa Baraza la Uamuzi wa Migogoro ya vyama vya
siasa, wapo walioona haja ya uwepo wake na wapo walipendekeza kuwa
majukumu ya Baraza hilo yafanywe na Baraza la Vyama vya siasa lililopo
sasa jambo lililosababisha kutokukubaliana katika hoja hiyo.
Pamoja na michango iliyotolewa ,
Wajumbe wameishauri Serikali kuona umuhimu wa kuwekeza katika Baraza la
Vyama vya Siasa ili kusaidia utatuzi wa migogoro nchini kwa kuwa
imebainika kuwa machafuko katika nchi nyingi duniani yamesababishwa na
machafuko katika masuala ya siasa.
Akihitaji ufafanuzi wa hatua
gani imefikiwa katika uboreshaji wa Sheria ya Vyama vya siasa,
Mwenyekiti wa Baraza la Vyama Vya Siasa, Mhe. Peter Kugar Mziray
aliiomba Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kutoa ufafanuzi. Naye
Msajili Msaidizi, Bw. Sisty Nyahoza akitoa ufafanuzi alisema tayari
vyama vyote vya siasa vimeshapelekewa barua vikiombwa kuwasilisha
mapendekezo kwa ajili ya kuboresha Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka
1992 na Sheria ya Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2010 na kwamba Ofisi
inafanya jitihada za kupokea mapendekezo kutoka kwa wadau wa siasa na
ikishakamilisha upokeaji huo, mapendekezo hayo yatawasilishwa kwenye
kamati ya Katiba na Sheria.
0 maoni:
Chapisha Maoni