Picha ikionyesha kaimu Katibu
Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akiwa anapokea kadi ya chadema na
kumkabidhi ya CCM alikuwa mgombea wa udiwani kata ya Kisimani kupitia
Tiketi ya chadema Amani John Mgonja Mara baada ya kuhamia Ccm.
Na Woinde Shizza , Kilimanjaro
Umoja wa Vijana wa
Chama cha Mapinduzi (UVCCM )umesema muda mfupi ujao Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo kitaifuata mahali viliko vyama vya
NCCR-Mageuzi, TLP na Chama cha Wananchi (CUF ) kwa sababu kimejidhuru
kukubali kukumbatia mafisadi .
Aidha umoja huo
umevitaja vyama hivyo sasa vinachechemea, vinaishi kwa matimaini na
viko mahututi kwani wakati wowote , ugonjwa uliovitafuna vyama hivyo
utakishambiulia chadema.
Matamshi hayo
yametamkwa leo na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka wakati
akizungumza na wanachama wa Uvccm na jumuiya zake katika mkutano wa
hadhara uliofanyika katika kijiji cha Maendeleo Kata ya Mabogini wilaya
ya Moshi vijijini.
Shaka alisema jeuri na
mbwembwe za NCCR ‘Mgeuzi, CUF na TLP muda umepita na sasa havina
mategemeao tena ya kuibuka na kushindana na chama tawala .
Alisema vyama hivyo
hupenda kujiita vyama vya siasa jambo ambalo alisema si kweli
kwasababu kujiendesha kwake kunamtegemea mtu badala ya kujijenga na kuwa
taasisi kamili.
Alisema vyama hivyo vineajua kutegemea makapi yaloachwa na ccm ili yawasaidie kuendesha masuala ya kisiasa .
Shaka akizungimza
katika mkutano huo alimtolea mfano mbunge wa Moshi vijijini Anthony
Komu (chadema) akisema hana uwezo wala uaminifu katika dhima ya
kuwatumikia wananchi kwasababu historia yake ya kisiasa haionyeshi kama
mtu madhubuti na mwenye msimamo.
“Komu alikuwa
mwanachama na kiongozi wa NCCR -Mageuzi tokea mwaka 1992 , akahama na
kujiunga Chadema akivutiwa na ukabila, wakati fulani akataka aende TLP
Mrema akamuwekea ngumu , aina ya kiongozi kama Komu ni ushahidi tosha
si kiongozi muaminifu , kesho sivajabu ukasikia amegama chadema
kurudi ccm “alisems Shaka
Hata hivyo Kaimu huyo
katibu Mkuu aliitaka halmashauri ya wilaya ya Moshi vijijini kufanya
kila linalowezekana kupekeka maji katika maeneo ya kata ya Mabogini ili
wananchi waondokane na adha ya ukosefu maji.
“Wananchi wa Moshi
vijijini nakuhalikishieni kuwa ujenzi wa barabara yenu umbali wa
kilomita 14 toka TPC hadi Chekereni itatekelezwa na serekali ya Dk
Magufuli kwa kiwango cha lami “alisema shaka.
Katika kijiji cha Chekereni kata ya mabogini wanachama wapya 34 wamejiunga na Uvccm, 27 CCM na UWT wanachama 12.
0 maoni:
Chapisha Maoni