Postedy by Esta Malibiche 0n 16 July 2016 in Jamii
Mkurugenzi
mawasiliano na Masoko wa kampuni ya saruji la Lafarge Tanzania Allan
Chonjo akiwaeleza wananchi wa kijiji cha Mpuguso kata ya Mpuguso
wilayani Rungwe mkoani Mbeya kwamba kampuni hiyo imetoa mifuko 150 ya
saruji kwa ajili ya ujenzi wa Kituo Cha Afya cha kata hiyo, kushoto ni
mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla.
Wakazi wa
kijiji cha Mpuguso wilayani Rungwe mkoani Mbeya wakishangilia baada ya
kupata taarifa za msaada wa saruji kutoka kampuni ya Lafarge Tanzania.
Mkuu wa
mkoa wa Mbeya Amos Makalla akipokea mifuko ya saruji kutoka kwa Maofisa
wa kampuni ya Lafarge Tanzania kwa ajili wa ujenzi wa Kituo cha Afya cha
kata ya Mpuguso kilichopo wilayani Rungwe mkoa wa Mbeya,(kushoto ni
Fundi Mshauri wa ujenzi wa gharama nafuu wa Lafarge Evarist
Mnyema,Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko Allan Chonjo na Meneja wa
Habari na Mahusiano Straton Bahati.
Mkuu wa
mkoa wa Mbeya Amos Makalla akishirikiana na viongozi wa Kijiji cha
Mpuguso kubeba mfuko wa saruji kati ya mifuko 150 iliyotolewa na kampuni
ya Lafarge Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kata
hiyo.
Mkuu wa
mkoa wa Mbeya Amos Makalla akitoa neno la shukurani mara baada ya
kukabidhi mifuko 150 ya saruji iliyotolewa na kampuni ya Lafarge
Tanzania, kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Mahusiano na Masoko wa Lafarge
Allan Chonjo, kulia ni Diwani wa kata ya Mpuguso.
Mkuu wa
Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akishiriki ujenzi wa Kituo cha Afya cha
Mpuguso wilayani Rungwe mkoani Mbeya mara baada ya kukabidhi mifuko 150
ya saruji iliyotolewa na kampuni ya Lafarge Tanzania.
Lafarge
Tanzania (Mbeya Cement Company), imetoa msaada wa mifuko mia moja
hamsini (150) ya saruji ya Tembo ikiwa ni msaada wake kuchangia ujenzi
wa kituo cha afya cha kijiji cha Mpuguso kilichopo wilayani Rungwe mkoa
wa Mbeya.
Akiongea
wakati wa makabidhiano ya msaada huo, Mkurugenzi wa Masoko na
Mawasiliano wa Lafarge, Allan Chonjo amesema “Lafarge Tanzania inaelewa
kwamba afya ndio kitu cha thamani zaidi katika maisha ya binadamu na kwa
sababu hiyo tumeona ni wajibu wetu kuchangia maendeleo ya jamii hii
ambayo tunayoishi. Tunasaidia ujenzi wa kituo cha afya Mpuguso kwakuwa
tunaelewa kwamba afya njema ndio msingi muhimu wa jamii kuweza kupata
maendeleo.”
Chonjo
alisema kwamba kampuni hiyo ya saruji inaamini kuwa biashara ni
kipaumbele chake lakini inaamini kwamba kusaidia jamii ni jukumu lake la
msingi. Msaada huo uliopokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kijijini
Mpuguso leo ni sehemu programu ya Lafarge Tanzania kusaidia jamii na
umelenga kuhakikisha ujenzi wa kituo hicho kinachojengwa na wananchi
unakamilika mapema ili kuboresha utoaji huduma za afya katika eneo hilo.
Akipokea
msaada huo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla alielezea kufurahishwa
kwake na Lafarge katika kuitikia wito wa wananchi haraka na kutoa msaada
huo. Mkuu huyo wa mkoa aliwahakikishia Lafarge kwamba msaada huo
utatumika ipasavyo kukamilisha mradi huo ili kuboresha maisha ya watu na
kuongeza kwamba kituo hicho kitahudumia maelfu ya wakazi wa Mpuguso na
maeneo ya jirani ambapo kituo cha karibu zaidi cha afya kipo umbali wa
takribani kilomita 60 kutoka eneo hilo.
Makalla
alisema kwamba baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho, wakazi wa
Mpuguso na maeneo ya jirani watapata huduma za msingi za afya ambazo ni
pamoja na ushauri wa kitabibu, msaada wa madawa, utoaji chanjo kuzuia
magonjwa mbalimbali pamoja na kutoa ushauri nasaha kuhusu afya.(P.T)
0 maoni:
Chapisha Maoni