|
WANAFUNZI
wa Chuo Kikuu cha St Joseph (SJUIT) Kampasi ya Arusha (kilichofutiwa
usajili), waliokuwa chini ya programu ya shahada ya miaka mitano ya
ualimu wa sayansi, wametakiwa kusoma ngazi ya cheti au stashahada. Kama
watataka kusoma ngazi ya juu, watapaswa kuomba upya udahili.
Aidha,
Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi imesema
wanafunzi waliokuwa wakipata mkopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa
Elimu ya Juu (HESLB), mikopo yao pia imesimamishwa.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi,
Profesa Simon Msanjila alitoa agizo hilo jana kupitia taaarifa kwa
vyombo vya habari. Profesa Msanjila alisema hatua hiyo, inatokana na
kubainika kwamba wanafunzi hao hawastahili kusoma shahada na pia
hawakustahili kupewa mkopo.
“Tunawafahamisha
wanafunzi wa SJUIT waliokuwa kwenye programu ya miaka mitano kwamba
watatakiwa kuishia daraja la cheti na stashahada... Kama wanafunzi hao
watataka kuendelea na masomo ya juu, watatakiwa kuomba upya,” ilisema
taarifa hiyo.
Februari
25, mwaka huu, Wizara kupitia Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) baada ya
kujiridhisha kuwa Kampasi ya Arusha ya Chuo Kikuu cha Mt. Joseph
Tanzania imepoteza sifa na vigezo vya kuendelea kutoa elimu ya chuo
kikuu, ilifuta kibali cha kuanzishwa kwake.
Iliidhinisha
uhamisho wa wanafunzi wote, waliokuwa wanasoma katika Kampasi hiyo ya
Arusha kwa gharama za Chuo Kikuu cha SJUIT. Aidha, ilifuta udahili wa
wanafunzi wapya katika programu ya shahada ya miaka mitano ya ualimu wa
sayansi.
Ilielekeza
wanafunzi waliokuwa wakiendelea na masomo katika programu hiyo,
wahamishiwe katika Kampasi ya Luguruni, Dar es Salaam. TCU ilielekeza
kwamba wanafunzi watalazimika kwanza kuhitimu katika ngazi ya Stashada,
kama ilivyokuwa imeidhinishwa na Tume hapo awali. Wanafunzi
waliohamishiwa kwenye vyuo mbalimbali, waendelee na masomo.
Taarifa
hiyo ilisema wakati wa mchakato wa uhamisho, wanafunzi wote walihakikiwa
kubaini kama wanakidhi vigezo vya kusoma kwenye ngazi hiyo. Wanafunzi
wote waliokuwa wakisoma programu hiyo ya miaka mitano, walihamishiwa
kwenye Kampasi ya Luguruni, jijini Dar es Salaam.
Hata
hivyo kutokana na mchakato wa uhakiki, baadhi ya wanafunzi walikutwa
hawana sifa za kujiunga na mafunzo hayo ya ualimu. Wale waliobainika
kuwa na sifa, walitaarifiwa kuendelea na masomo kwenye kampasi hiyo ya
Luguruni.
Wanafunzi
katika kundi hili waliobainika kuwa na vigezo, walitaarifiwa kuendelea
na masomo katika Kampasi ya Luguruni. Maana ya kuwa na vigezo vya ufaulu
tunavyovizungumzia hapa ni kwamba wanafunzi husika wamefaulu katika
masomo lengwa yanayowawezesha kusoma Cheti cha Ualimu Daraja “A” ambacho
ni kigezo cha kwanza kwa mujibu wa mtaala wa programu hiyo.
0 maoni:
Chapisha Maoni