PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.
……………………………………………………………………………….
Na Shamimu Nyaki-WHUSM.
Waziri wa Habari Utamaduni,Sanaa
na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye amezindua studio ya redio ya jamii ya
‘Community Media Network of Tanzania’ (COMNET) katika Chuo kuku Huria(
OUT ) itakayotumika kusambaza habari maeneo yenye uhaba wa redio.
Uzinduzi huo umefanyika leo
jijini Dar es Salaam,ambapo Mhe. Waziri amesema kuwa studio hiyo
itasaidia idadi kubwa ya wanachi wanaoishi vijijini kupata habari
kutoka Serikalini na kutoa mrejesho wa kile watakachosikia kwa urahisi.
“Ni Studio muhimu kwa ajili ya
kusambaza demokrasia kwa watu hasa wale waliopo vijijini kwa vile redio
nyingi bado hazijawafikia”Alisema Mhe.Nape.
Aidha amewataka wanafunzi wa
taaluma ya uandishi wa habari na mawasiliano kwa umma katika chuo
hicho kutumia studio hiyo kujifunza zaidi kwa vitendo na kuzingatia
maadili ya uandishi wa habari kwa kuandika habari zenye ukweli kutoka
vyanzo sahihi ili kutoa ujumbe wenye manufaa mazuri kwa jamii.
Kwa upande wake Makamu mkuu wa
Chuo hicho Prof. Elifas Bisanda amesema studio hiyo imeanzishwa kwa
ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na
Utamaduni(UNESCO) kwa lengo kutoa elimu kwa jamii ambayo imekuwa
haipati habari kwa urahisi.
Amewataka wanahabari na wananchi
kwa ujumla kufikisha habari katika studio hizo kwa kuwa inatumia njia
ya haraka na rahisi katika kufikisha ujumbe kwa kushirikiana na redio
mbalimbali za jamii.
Naye mwakilishi kutoka Shirika la
umoja wa mataifa linaloshughulikia Elimu,Sayansi,na Utamaduni(UNESCO)
Bi. Zulimira Rodrigues amesema studio ya redio ya ‘Community’ ipo kwa
ajili ya kutoa elimu kwa jamii kuhusu maendeleo ya wanawake na vijana
ambao ndio nguvu kazi ya Taifa.
Mpaka sasa Shirika hilo
limefanikiwa kuanzisha redio za jamii katika baadhi ya mikoa ya Tanzania
bara ambayo ni Mwanza,Arusha na Tanga na katika baadhi ya maeneo ya
Unguja na Pemba.
0 maoni:
Chapisha Maoni