Dada
Regina Tarimo Afisa uhusiani wa TAZARA-Tanzania, akiwakaribisha
wajumbe wa Baraza hilo jipya kwenye mkutano maalum wa uzinduzi wa Baraza
Kuu la Wafanyakazi wa TAZARA unaondelea jijini Dar es Salaam katika
hoteli ya Lamada, leo Juni 25.2016.
Baadhi
ya wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa TAZARA wakifuatilia mkutano
huo unaondelea jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Lamada, leo Juni
25.2016.
Baadhi
ya wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa TAZARA wakifuatilia mkutano
huo unaondelea jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Lamada, leo Juni
25.2016

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Nicholas Mgaya akisoma taarifa namna ya TUCTA inavyofanya kazi na Mabaraza ya wafanyakazi sehemu za kazi.
Baadhi
ya wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa TAZARA wakifuatilia mkutano
huo unaondelea jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Lamada, leo Juni
25.2016
Baadhi
ya wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa TAZARA wakifuatilia mkutano
huo unaondelea jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Lamada, leo Juni
25.2016
Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo upande wa Uchukuzi, Dk Leonard Chamuriho akisoma
hutuba hiyo ya ufunguzi kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo, Profesa
Makame Mabarawa.

Mkuu wa Wizara hiyo upande wa Uchukuzi, Dk Leonard Chamuriho (mbele)
akisoma hutuba hiyo ya ufunguzi kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo,
Profesa Makame Mabarawa.
Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo upande wa Uchukuzi, Dk Leonard Chamuriho akisoma
hutuba hiyo ya ufunguzi kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo, Profesa
Makame Mabarawa.
Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo upande wa Uchukuzi, Dk Leonard Chamuriho(wa pili
kutoka kulia) akipiga picha ya pamoja na viongozi wa juu wa wafanyakazi
wa TAZARA. Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo upande wa Uchukuzi, Dk Leonard Chamuriho (Katikati)
akipiga picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza jipya la Wafanyakazi wa
TAZARA. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa. Makame Mbarawa (MB)
amezindua rasmi Baraza Kuu la kwanza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya reli
ya Tanzania na Zambia (TAZARA) tukio lililofanyika mapema leo Juni
25.2016, Jijini Dar es Salaam.
Akisoma
hutuba ya ufunguzi wa Baraza hilo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo upande
wa Uchukuzi, Dk Leonard Chamuriho kwa niaba ya Waziri Profesa Mbarawa,
Amelitaka Baraza hilo kufanya kazi kwa moyo mmoja katika hali ya
kuifufua TAZARA kiutendaji na ufanisi kama ilivyokuwa zamani.
Akisoma
hutuba hiyo, aliwapongeza viongizi wa wanaounda Mamlaka hiyo akiwemo
Mhandisi Bruno Ching’andu kwa kuteuliwa kwake kuongoza Mamlaka ya Reli
ya Tanzania na Zambia na viongozi wengine pamoja na wafanyakazi wote.
Ambapo
alisema kuwa, ni dhahiri hatua ya leo imefikiwa baada ya jitihada kubwa
na hasa tukitilia maanani hali ya kifedha ambayo TAZARA inapitia katika
kipindi hiki. Hivyi kuwapongeza kwa uamuzi huo kwani Mabaraza yana
umuhimu mkubwa katika maeneo ya kazi na yameonyesha mafanikio makubwa
kila yalipoanzishwa kwani yameweza kuongeza uhusiano mwema kati ya
Manejimenti, Vyama vya Wafanyakazi na wafanyakazi kwa upande mwingine.
“Mabaraza
haya ni dhana ya ushirikishwaji ikiwa na maana kuwapatia wafanyakazi
fursa ya kushauri juu ya masuala ya utendaji kazi, sera za taasisi,
ufanisi wa kazi, mazingira ya kazi, ustawi wa wafanyakazi katika elimu,
nidhamu, vyeo, pamoja na motisha kwa wafanyakazi. Pia dhana hii ya
ushirikishwaji ni kwa mujibu wa sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya
mwaka 2002 na kanuni zake za mwaka 2003 kifungu cha 108.
Pia
ni kwa mujibu wa Sheria ya majadiliano katika Utumishi wa Umma Na. 19
ya mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2005. Pia Sheria ya ajira na
mahusiano kazini ya mwaka 2004 na kanuni zake za mwaka 2007 kifungu Na.
73 (1 - 3).
Taarifa
niliyopewa ni kwamba kikao hiki cha sasa cha Baraza kitapata fursa ya
kuijadili taarifa ya kazi ya Mamlaka kwa mwaka 2015/2016, kuupitia
mpango kazi kwa kipindi cha 2016/2017 na pia bajeti ya mapato na
matumizi ya Mamlaka kwa kipindi cha mwaka 2016/2017. Kwa maana hiyo hiki
ni kikao muhimu sana kwa mustakabari wa Mamlaka ya TAZARA.
Wajumbe
wote ninawaomba muwe makini sana kuelewa hayo malengo na kuweza
kutafsiri kwa usahihi ili muweze kuyawakilishe hali halisi kwa
wafanyakazi wenzenu kwa ili malengo yapate kutimizwa. Ninyi mtakuwa
kiungo muhimu sana katikakufanikisha swala zima la kuleta matumaini
mapya.
Kwa
kuwa Mamlaka hii ni alama ya ushirikiano baina ya Tanzania na Zambia
imeendelea kuwa muhimu kwa nchi zetu. Napenda kuwakumbusha wajumbe wote
kwamba wajibu wenu kwa sasa ni kuhakikisha Mamlaka inarudi katika hali
yake ya zamani ilipokuwa ikijiendesha yenyewe kwa kutimiza wajibu wake
wa kulipa mishahara kwa wafanyakazi,kulipa kodi Serikalini, michango ya
wafanyakazi katika mufuko ya jamii ..
Na
kwa njia hii pekee itayorudisha imani upya kwa wateja ambao wamejiondoa
kwa kipindi sasa hali iliyopelekea hali ya Mamlaka kimapato kudhoofika.
Kwa
kumalizia, napenda nitoe rai kwa uongozi wa Mamlaka na wa vyama vya
Wafanyakazi kuwa mkutano huu uwe ni mwanzo muendelezo wa mikutano
mingine kadri kanuni inavyoagiza ili kuongeza tija na utulivu. Mahali
hapa ni fursa ya kuelezana, kukosoana na kuwekana sawa kwa manufaa ya
TAZARA na Umma wote wa Tanzania na wa Zambia pamoja na nchi jirani
wanaotumia reli hii kwa namna moja au nyingine.
Mwisho nawatakia mkutano wenye mafanikio na pia napenda kutangaza kwamba Baraza hili nimelizindua rasmi. Ahsanteni!
0 maoni:
Chapisha Maoni