Mkurugenzi wa Mazingira wa SABMiller Africa,Muzi Chonko katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
———————————————————–
Na Mwandishi wetu
Kampuni ya kimataifa ya SABMiller
inayomiliki viwanda vya kutengeneza vinywaji sehemu mbalimbali duniani
itaendelea kufanya biashara zenye mwelekeo wa kubadilisha maisha ya
jamii mbalimbali kuwa bora bila kusahau kuzingatia utunzaji wa
mazingira.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi
wa Mazingira wa kampuni hiyo kanda ya Afrika Bw.Muzi
Chonco,alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo
alipata wasaa wa kuelezea kanuni zinazoongoza utendaji wa kazi wa
kampuni kwa ajili ya kuleta mabadiliko endelevu sehemu zote ilikowekeza
duniani.
Chonco alisema kuwa tangu kampuni
ianze kutumia kanuni hizo ambazo zinashahabiana na malengo ya umoja wa
mataifa tayari mafanikio mbalimbali yameanza kupatikana na yapo
matumaini ya kufikia mafanikio makubwa katika siku za usoni.
“Tunapoongelea biashara endelevu
tunamaanisha kuwawezesha wanachi kiuchumi kama ambavyo tumekuwa
tukifanya kazi na wakulima kupitia mpango wetu wa Go Farming,kuwakwamua
wanawake kiuchumi,kuendeleza wajasiriamali,kutunza vyanzo va maji na
kuwekeza katika miradi ya maji bila kusahau utunzaji wa
mazingira”.Alisema Chonco.
Alitoa mfano wa kampuni ya TBL
Group ambayo iko chini ya kampuni hiyo kwa jinsi ilivyoweza kufanya
uwekezaji ambao umeleta mabadiliko nchini ambapo serikali na taaasisi
mbalimbali zinatambua mchango wake kwa kuitunukia tuzo mbalimbali ambazo
imekuwa ikishinda mwaka hadi mwaka.
Chonco alizichambua kanuni
zinazoongoza kampuni na kuleta mabadiliko kwenye jamii kuwa ni dunia
yenye nuru njema,dunia changamfu,dunia imara,dunia iliyo safi na dunia
yenye nguvu kazi.
Alisema wakati umefika kwa
wawekezaji mbalimbali kufanya uwekezaji wenye kuleta mabadiliko kwenye
jamii badala ya kunufaisha upande mmoja “uwekezaji unaoleta ajira za
kila aina kwa wananchi,unaowawezesha kujipatia mapato kwa kuuza bidhaa
kwa kampuni iliyowekeza,kutunza mazingira na kuwapatia wananchi elimu ya
utunzaji wa mazingira na vyanzo vva maji,kusaidia makundi mbalimbali
kwenye jamii yaliyoachwa nyuma ukizingatiwa kwa vyovyote utaleta
mabadiliko”.Alisisitiza.
Alitoa mfano kuwa ukimwezesha
mkulima ataweza kupata kipato na kujenga nyumba nzuri ya kuishi,watoto
wake kusoma vizuri,familia yake kupata lishe bora na kuongeza pato la
familia kwa ujumla na maisha kubadilika kutoka hali duni kuwa bora kama
ambavyo imetokea kwa wakulima na makundi mengine yanayoshirikiana na
kampuni hiyo sehemu mbalimbali duniani.
0 maoni:
Chapisha Maoni