Serikali
ya Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya
Kimataifa ya Mazingira na Maendeleo (IIED), Mfuko wa Umoja wa Mataifa
wa Maendeleo (UNCDF LoCAL) na mashirika mawili yasiyokuwa ya kiserikali
ambayo ni Haki Kazi catalyst (HKC) na Jumuiko la Maliasili Tanzania
(TNRF) wamezindua mradi wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na
tabianchi wazinduliwa.
Mradi
huo kwa mara ya kwanza ulianza kwa majaribio kati ya mwaka 2012 hadi
2013 katika Halmashauri tatu (3) za wilaya za Longido, Ngorongoro, na
Monduli Mkoani Arusha.
Baada
ya awamu hiyo ya majaribio kumalizika na kuonesha mafanikio makubwa
mradi huo umerejea tena awamu hii ukihusisha Halmashauri nyingine 12
katika mikoa ya Manyara, Tanga, Kilimanjaro, Pwani, Lindi na Dodoma na
utasimamiwa na TAMISEMI kwa msaada wa kiufundi na rasilimali fedha
kutoka kwa serikali ya Uingereza (UK-AID) na Mfuko wa Umoja Wa mataifa
wa maendeleo (UNCDF).
Mradi
huu umepangwa kutekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano (2016-2021)
ambapo awamu ya kwanza itaanza kutekelezwa kuanzia mwaka huu 2016-2018
na awamu ya pili ikianza mwaka 2018-2021.
Kupitia
mradi huo unalenga kuijengea uwezo Ofisi ya Raisi –TAMISEMI katika
maene makubwa mawili ambayo ni uimarishaji wa taasisi katika uratibu wa
mradi na uwezo wa kutafuta rasilimali fedha kwa ajili ya kuziwezesha
mamlaka za serikali za mitaa hapa nchini ziweze kutoa elimu kwa jamii
kutambua na kutekeleza Miradi ya kukabiliana na athari ya mabadiliko ya
hali ya hewa na tabianchi.
Katibu
mkuu wa TAMISEMI, Musa Iyombe aliyemwakilisha Waziri wa TAMISEMI,
Goerge Simbachawene katika uzinduzi huo, anasema kuongezeka kwa athari
za mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi sasa ni tatizo kubwa na
tayari yamelta madhara makubwa katika maisha ya binadamu na pia katika
uchumi wa taifa na kuleta mzigo mkubwa kwa taifa la Tanzania.
Tazama hapa tukio hilo:
Alais Morindat, Mwakilishi Msahuri wa Taasisi ya Kimataifa ya Mazingira na Maendeleo (IIED), (IIED) akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo
Lucy Ssendi, Mkurugenzi Msaidizi, TAMISEMI, akizungumza na mwandishi wa habari hizi wakati wa uzinduzi wa mradi huo
Kunizio Manyika, Afisa Misitu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo
Katibu
mkuu wa TAMISEMI, Musa Iyombe akishikana mkono na Fakri Karim, Meneja
Program kutoka Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo (UNCDF LoCAL)
mara baada ya kusaini makubaliano ya utekelezaji wa mradi wa kukabiliana
na mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi
0 maoni:
Chapisha Maoni