DSC_4628
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye akitoa hotuba katika halfa uzinduzi wa studio katika Chuo Kikuu Huria (OUT).
Nae Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini, Zulmira Rodrigues alisema UNESCO imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kuzisaidia redio za kijamii ili ziweze kufanya kazi kwa ufanisi kwa kutambua kuwa redio hizo zina umuhimu katika maeneo ambazo zinakuwepo kwa kuripoti habari ambazo zinaihusu jamii husika.
DSC_4600
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi au Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza kwa niaba ya UNESCO jinsi inavyozisaidia redio za kijamii.
Kwa upande wa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Prof. Elias Bisanda, aliwakaribisha wanahabari wa redio za kijamii chuoni hapo na kueleza kuwa redio za kijamii zimekuwa na changamoto mbalimbali ambazo zinatakiwa kufanyiwa marekebisho ikiwepo pamoja na kuwa na vipindi vya kujitoshereza na kuacha kuwa wakitegemea vyombo vingine vya habari kujiunga nao ndiyo kuwepo hewani.
DSC_4557
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Prof. Elias Bisanda akielezea kuhusu utendaji kazi wa redio za kijamii.
DSC_4567
Akielezea kuhusu vipindi vitakavyozalishwa katika studio hiyo, Mwenyekiti wa Mtandao wa Redio za Jamii Tanzania (COMNETA), Joseph Sekiku alisema vipindi vitakuwa vikitengenezwa na kuwekwa mtandaoni kisha redio jamii zitakuwa zikichukua vipindi katika mtandao huo kisha kuvitumia.
DSC_4568
Mwenyekiti wa Mtandao wa Redio za Jamii Tanzania (COMNETA) akizungumza jinsi ambavyo redio za kijamii zitakuwa zikipokea vipindi kutoka katika studio hiyo kwa ajili ya kuvitumia.
DSC_4542
Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Mohammed Mkonongo akizungumza kuhusu uzinduzi wa studio.
DSC_4648
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye akikata utepe kuashiria ufunguzi wa studio hiyo.
DSC_4674
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye akifanyiwa ‘interview’ baada ya kufanya uzinduzi wa studio hiyo.
DSC_4681
DSC_4695
Baadhi ya vifaa vinavyotumika katika studio hiyo kwa ajili ya kurekodi vipindi.
DSC_4550
Baadhi ya watu waliohudhuria halfa hiyo.
DSC_4549

Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) wamefanya uzinduzi wa studio ambazo zitakuwa zikitumiwa na waandishi wa habari wa redio jamii ambao watakuwa wakipata mafunzo katika chuo hicho, ufunguzi ambao umefanywa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri Nape amesema kuwa redio jamii zina umuhimu mkubwa katika jamii hasa kutokana na kuwa na habari nyingi ambazo zinakuwa za eneo husika tofauti na vyombo vya habari vya kitaifa ambavyo zinakuwa zinaripoti habari kutoka kila sehemu.
Waziri Nape aisema pamoja na umuhimu zilionao lakini bado zimekuwa na changamoto mbalimbali lakini uwepo wa studio hizo zitawezesha utengenezwaji wa vipindi bora ambavyo vitakuwa vikitumiwa na redio za kijamii.
“Redio hizi za kijamii zina sifa za kipekee katika kuripoti habari zake tofauti na redio zingine wasikilizaji wanapata nafasi ya kusikiliza habari kutoka eneo lao lakini pia kuna maeneo vyombo vya kitaifa havifiki ila zenyewe zinafika kwahiyo tutegemee studio hii itasaidia ubora wa vipindi vitakavyotumiwa na redio hizo,” alisema Nape.