Naibu
Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI ameziagiza Halmashauri za wilaya, Miji,
Majiji pamoja na Manispaa nchini kuhakikisha majengo ya Halmashauri zao
yanakuwa na hati miliki ili kuondoa migogoro kati yao na wananchi wenye
tabia ya kuvamia maeneo kwa visingizio ni mali ya familia zao.
Waziri
Jaffu alitoa agizo hilo katika Mji mdogo wa Nduguti,wilayani Mkalama
wakati wa kutembelea na kukagua majengo ya ofisi za Mkuu wa wilaya
pamoja na majngo ya ofisi za makao makuu ya Halmashauri ya wilaya ya
Mkalama.
Aidha
Waziri Jaffu alisema kwenye maeneo mengi alikofanya ziara zake alibaini
kwamba Halmashauri nyingi hazina hati miliki,jambo ambalo linaloweza
kusababisha wajanja wachache kutokea na kutengeneza hati bandia za
kuhalalisha maeneo hayo kwamba yalikuwa mali za babu zao.
“Hapa
nimeshalizungumza pale nilipofika nimeambiwa hapa kuna takribani mita
sguare hamsini ambao ukiugaanya kwa 4,060 kwa karibu sguare mita moja
unazungumzia takribani ekari 12”alifafanua Jaffu.
“Ekari
12 na nikatoa maagizo kwamba katika sehemu mbali mbali zilizopita
Halmashauri nyingi hazina hati miliki na mwisho wa siku ni kwamba
watatokea wajanja watadai kwamba yale majengo ya serikali ni maeneo ya
babu zao na inawezekana watu wakaja na suala zima la kuchonga hata hati
feki hapo baadaye”alisisitiza Naibu waziri huyo.
Kwa
hali hiyo kutokana na hofu hiyo Jaffu alitumia fursa ya ziara hiyo ya
wilayani Mkalama kuziagiza Halmashauri zote ziwe na hati miliki za
majengo yao.
Naibu
waziri huyo alikwenda mbali zaidi kwa kusema kuwa siyo hati miliki za
majengo ya Halmashauri hizo peke yake bali akasisitiza pia ni vyema pia
taasisi za serikali vikiwemo vituo vya afya pamoja na shule za msingi na
sekondari zilizopo kwenye maeneo yao.
Hata
hivyo Jaffu ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Kibaha alibainisha kwamba
kutokana na majengo hayo kutokuwa na hati miliki,kumechangia baadhi ya
shule za msingi na hata sekondari kuanza kuvamiwa na wananchi kutokana
na kile walichodai kuwa ni maeneo ya kwao na hata viwanja vya michezo
kukosekana.
“Manake
watu wamevamia kutokana na kutokuwa na hati miliki,kwa hiyo
nilikuagiza afisa ardhi kwamba hakikisha kwamba ajira yako ya kwanza
kuwe na hati miliki ya jengo hili”alibainisha Naibu waziri huyo.
Akisoma
taarifa ya ujenzi wa majengo ya utawala ya Halmashauri hiyo,Mhandisi wa
Ujenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkalama,Ramadhani Mohamedi alisema
ujenzi huo ulioanza mwanzoni mwa mwaka huu unatarajiwa kukamilika
sept,mwaka huu na kuelezea changamoto zinazoukabili ujenzi huo.
Alisema
katika kipindi cha mwaka 2014/2015 Halmashauri hiyo ilitengewa jumla ya
shilingi milioni 450 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la ofisi za
Halmashauri ya wilaya ya Mkalama baada ya kuwa imepokea kiasi hicho
kidogo cha fedha za mwaka 2013/2014.
Kwa
mujibu wa Mhandisi huyo wa wilaya ujenzi wa jengo la ofisi ya
Halmashauri ya wilaya ya Mkalama kwa awamu ya hiyo ya kwanza unakadiriwa
kutumia shilingi 758,180,798/= na hiyo ikiwa ni pamoja na kodi ya
ongezeko ya thamani,(VAT) ambayo ni karibu shilingi milioni na kitu.
“Mh
Naibu Waziri ujenzi wa jengo hili ulianza januari,21,2016 na
tunatarajia kuwa utakamilika sept,21,mwaka huu kwa awamu hii ya kwanza
kwa maana itatumia miezi minane”alifafanua zaidi.
Katika
hatua nyingine,kufuatia agizo la Rais John Pombe Magufuli la
kuhakikisha ifikapo juni,30,mwaka huu kila Halmashauri inaondokana na
tatizo la wanafunzi kukaa chini Kaimu afisa elimu msingi wa wilaya
hiyo,Nasibu Pangahela alisema Halmashauri hiyo ilikuwa na upungufu wa
madawati 14,840 na mpaka sasa imekamilisha utengenezaji wa madawati hayo
yote kwa hali hiyo hapatakuwa na mwanafunzi atakaykaa chini katika
wilaya hiyo.
Wakati
wa ziara yake ya siku moja wilayani Mkalama,Naibu Waziri Jaffu
ametembelea na kukagua majengo ya ofisi ya mkuu wa wilaya,majengo ya
utawala ya Halmashauri ya wilaya, kupokea madawati,kutembelea barabara
ya Msingi-Yulansoni hadi Iguguno yenye urefu wa kilomita 25.
Mbunge
wa jimbo la Iramba mashariki,Bwana Allani Kiullah akipokea taarifa ya
utengenezaji wa madawati kutoka kwa kaimu afisa elimu wa wilaya ya
Mkalama,Bwana Nasinu Pangaahela.
Mbunge
wa jimbo la Iramba mashariki,Bwana Allani Kiullah (wa kwanza kutoka
kulia) akimkabidhi Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI,Bwana Selemani
Jaffu madawati
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI,Bwana Selamni Jaffu(wa pili kutoka
kushoto) akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Mbigigi,Bwana
Donatus Lazaro (Aliyevaa shati la kitenge) kwa niaba ya walimu wengine
wa wilaya hiyo jumla ya madawati mia moja yaliyochongwa na Mbunge wa
jimbo la Iramba mashariki,Bwana Allan Kiullah kwa fedha za mfuko wa
jimbo.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)
0 maoni:
Chapisha Maoni