Serikali
kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ,
imesitisha tamko la utoaji wa vyakula kwa wagonjwa watakaolazwa katika
hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili kupisha utafiti wa kina kuhusu
huduma hiyo ili kuweza kutoa kilicho bora kwa watanzania.
Akizungumza
hayo leo jijini Dar es salaam Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Ummy Mwalimu amesema kwamba wameamua
kusitisha mpango mpaka watapotangaza tena ili kufanya utafiti kujua kama
kuna faida au hasara kwa wananchi.
“Natoa
tamko kwamba huduma hii iliyotarajiwa kuanza hivi karibuni isitishwe
mara moja ili kupisha watafiti waweze kufanya uchunguzi kujua
inawasaidia kwa kiasi gani wananchi,” alisisitiza Mh. Mwalimu.
Aidha
Bi. Mwalimu amesema kwamba huduma hiyo itatolewa kwa wagonjwa
watakaolazwa hapo kwa kulipia shilingi elfu 50 ikiwemo shilingi elfu
kumi ya kumuona daktari , elfu kumi ya kitanda na elfu 30 iliyobaki ni
kwa malipo ya chakula kwa wiki.
“Huduma
hii inalenga kuwasaidia wananchi katika kuwaandalia chakula stahiki kwa
wagonjwa na kupunguza usumbufu kwa waangalizi wa wagonjwa wao kuleta
vyakula hospitalini ili kuimalisha afya zao kwa ujumla,” aliongeza
Bi.Mwalimu.
0 maoni:
Chapisha Maoni