Kaimu mkuu wa mkoa wa Iringa ambae ni mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amewataka Maafisa lishe mkoani hapa kuwasilisha taarifa ya lishe ya chakula ya wananfunzi wa shule za msingi ofisini kwake kabla ya tarehe 30/6/2016
Akifungua kikao cha
wadau wa maendeleo mkoa wa Iringa kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa
Iringa,mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela alisema katika takwimu, mkoa unaongoza kwa udumavu wa watoto
wenye umri chini ya miaka 5 hawana lishe.Halii hii inatokana na wazazi kuwa wazembe na kushindwa kuzinagtia Elimu ya Afya inaypotolewa katika vituo vya
afya.
Kasesela alisema mkoa wa Iringa ni miongoni mwa mikoa
inayozalisha chakula kwa wingi ingawa bado unakabiliwa na changamoto ya ukosefu
wa lishe kwa watoto na akina mama wajawazito hali inayopelekea udumavu.
Hali hiyo inatokana na wazazi kutokuwa karibu na watoto
wao,kujikita zaidi katika shughuli za biashara na ulevi na kushindwa kuzingatia Afya ya lishe kwa
watoto.
‘’’Ingawa mkoa wetu unazalisha chakula kwa wingi lakini
changamoto ya watoto kukosa lishe na kusababisha udumavu ni mkubwa.wazazi
tunatakiwa tuzingatie Afya kwa watoto ili mka uweze kuondokana na hali ya
udumavu kwa watoto.
Aidha Kasesela alisema hali ya madawati kwa mkoa wa Iringa karibu
wilaya zote zimetekeleza na zinaendelea kutekeleza ingawa changamoto ipo kwa watengenezaji
lakini hadi tarehe 30/6/2016 kama agizo la Mh.Rais linavyosema yatakuwa
yamekamilika ili watoto watakaporejea shuleni wakute madawati yako tayari
Kwa upande wake Afisa lishe wa Mkoa wa Iringa Sizo Nzogere
alisema pamoja na mikoa ya Iringa na
njombe ni miongoni mwa mikao
inayozalisha chakula kwa wingi ,lakini kuna tatizo la kubwa la udumavu kutokana na hali ya lishe
kuwa duni. Kila siku watoto 130 wanakufa
pamoaja na akina mama 1600 kwa mwaka
wanakufa kutokana matatizo ya utapia mlo.hii inatokana na uwezo mdogo
wa kutozingatia umuhimu wa lishe.
Nzogere alisema mikakati iliyowekwa na mkoa ili kuhakikisha
akina mama wajawazito wanazingatia swala la lishe ni pamoja na kuwajengea uwezo
wahudumu wa afya ili waweze kutoa Elimu sahihi ya lishe katika vituo vya
kutolea huduma za afya.Kuendeshwa kwa
kamati ya lishe katika Halmashauri zote zinazowahusisha viongozi wa dini
kujadili mikakakti na changamoto mbalimbali za lishe ili kutokomeza hali ya
udumavu kwa katika mkoa.
Aidha alisema ili kuzuwia uatapia mlo katika mkika wa
Iringa Elimu inatakiwa itolewe kwa wananchi ili mama mjamzito toka mimba
inatungwa aweze kuzingatia swala la
lishe ili kumlinda motto wake akiwa tumboni hadi kuzaliwa.
‘’’’’’’’’’ Jumal ya
vifaa 610 vya kupimia hali ya lishe kwa watoto walio chini ya umri wa miaka
mitano vimesambazwa katika
Halmashauri.Utoaji wa Elimu lishe,madini joto,ulaji unaofaa,viatamini A ,dawa
za minyoo,unyeshaji ulishaji watoto wadogo na wachanga na
inaendelea kutolewa kwa wazazi
/walezi kila siku katika vituo 217
vinavyotoa huduma ya mama na motto ambapo hadi sasa walezi 129839 wamepokea
Elimu lishe katika kipindi cha
januari,May’’’’’’’alisema…..
Pascal Nsana ni miongoni mwa wadau wa maendeleo waliohudhuria
kiao hicho cjha wadau wa maendeleo nae
alisema kuwa changamoto kubwa iliyopo katika lishe inatokana na wananchi
kutokyua na Elimu tya kutosha kuhusu umuhimu wa kuzingatia lishe .
‘’’’Mkoa unachakula cha kutosha namna ya kuandaa chakula na kuzingatia
lishe Elimuinatakiwa kutolewa juu ya
makundi matono ya chakula yanayotakiwa kuzingatiwa mara mama anapokuwa mjamzito
na baada ya kujifungua na jamii kwa ujumla’’’’’’alisema
0 maoni:
Chapisha Maoni