Picha na: Nasra Mwangamilo, TAMISEMI
———————————————————
Halmashauri nchini zatakiwa
kufanya kazi kwa weledi na ufanisi ili kuleta matokeo chanya na kwa
wakati, huku wakijiepusha na ufujaji rasilimali za umma wakati wa
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikaliza Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhandisi
Mussa Iyombe alipokuwa akimwakilisha Waziri wa nchi OR – TAMISEMI Mhe.
George Simbachawene katika uzinduzi rasmi wa mradi wa Kukabiliana na
Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabia nchi (Decentralized Climate Finance
in Tanzania) leo mjini Dodoma.
“Niseme tu kuwa nategemea utendaji
wenye matokeo chanya kwa kufanya hiyvo kutajenga imani kwa wafadhili,
Wakurugenzi wote nchini fanyeni kazi kwa weledi,ufanisi na muepuke
kufuja mali za umma” Alisema Mhandisi Iyombe.
Mhandisi Iyombe aliongeza kuwa
mradi huu umelenga kuwajengea uwezo wanajamii katika kukabiliana na
athari za mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi ambapo juhudi
mbalimbali zimekuwa zikifanyika katika kukabiliana na hilo.
Serikali kwa kushirikiana na wadau
wa maendeleo hususan Shirika la Kimataifa la Mazingira na Maendeleo
(IIED), Haki Kazi Catalyst (HKC), Jumuiko la Maliasili Tanzania(TNRF)
chini ya ufadhili wa Serikali ya Uingereza (UK-aid) na Mfuko wa Umoja wa
Mataifa wa Maendeleo (UNCDF LoCAL) itatekeleza mradi huu katka
Halmashauri 15 nchini.
Halmashauri hizo ni pamoja na
Kondoa, Bahi, Manyoni, Mpwapwa, Kiteto, Same, Simanjiro, Kilwa, Siha,
Mbulu, Iramba na Pangani ambazo zimejumuishwa na Halmashauri za Monduli,
Ngorongoro na Longido zilizokuwa katika mradi wa majaribio.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu
anyeshughulikia Afya kutoka OR-TAMISEMI Deo Mtasiwa amesema kuwa kwakuwa
Serikali tayari imekwisha tengeneza mfumo imara ilikuhakikisha
utekelezaji wa mradi huo unafanikiwa kuanzia ngazi ya kijiji.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa
mradi huu MwakilishiMshauri wa Taasisi ya Kimataifa ya Mazingira na
Maendeleo (IIED) Alais Morindat alisema kuwa mabadiliko ya hali ya hewa
siyo kitu kipya na kuongeza kuwa historia ya mradi huo inatokana na
athari zilizojitokeza katika jamii za wafugaji katika maeneo ya
Kasikazini mwa Tanzania ambapo mifugo mingi katika maeneo ya Monduli,
Ngorongoro na Longido ilipoteza uhai.






0 maoni:
Chapisha Maoni