———————————-
JAMII imeshauriwa kubadilisha
mfumo wa kupenda kukaa nje ya nyumba zao kwa ajili ya mazungumzo hasa
nyakati za usiku ili kuepuka kupata maambukizo ya ugonjwa wa malaria .
Mkuu wa kitengo cha
kudhibiti ugonjwa wa malaria Pemba Bakar Omar Khatib alitoa ushauri huo
wakati akizungumza na maafisa wa Wizara ya afya kutoka Wilaya ya
Micheweni na Wete kwenye mkutano wa uhamasishaji zoezi la utoaji wa
vyandarua vilivyotiwa dawa uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha
uwalimu Benjamini Mkapa.
Amesema kwamba utafiti
uliofanywa na wataalamu wa kitengo hicho umebaini kwamba mbu
anayesababisha malaria hupenda kukaa nje ya nyumba na kwamba njia ya
kukabiliana na ugonjwa huo ni kwa jamii kuachana na tabia ya kukaa nje
kufanya mazungumzo .
“Mbu anayesababisha malaria nao
ni wajanja wanapenda kukaa nje , hivyo ili kukabioliana na ugonjwa huu ,
ni vyema jamii kubadilisha mfumo wa kukaa ya nje ya nyumba zao kwa
ajili ya mazungumzo ”alifahamisha.
Aidha amesema kwamba kutokana na
hali hiyo , walio katika hatari ya kupata maambulizi ya ugonjwa huo
zaidi ni watu wazima kuliko watoto kwani ndiyo wanaopenda kukaa nje ,
hususani kwa kuangalia TV na mazungumzo .
Nao washiriki wa kikioa hicho
wamekishauri kitengo hicho kuzungumza na makampuni ya simu za mikononi
ili yatumike kusambaza ujumbe ka wamiliki wa simu unaotambulisha
matumizi sahihi ya vyandarua .
Juma Shaame Salim kutoka mamlaka
ya usimamizi wa mazingira Wilaya ya Wete , alisema utaratibu huo
utasaidia kufikisha ujumbe kwa wananchi kwa wakati muafaka kutokana na
idadi kubwa ya wananchi wanamiliki ya simu za mikononi
“Kutokana umuhimu wa suala hili
, ni vyema kitengo hichi kuzungumza na makampuni wa simu za mikononi
ili yasaidie kueneza ujumbe kwani wananchi wengi wanamiliki simu za
mikononi ”alishauri .
Naye Ali Rajabu kutoka Wilaya ya
Micheweni akichangia kaatika mkutano huo aliomba kitengo kuandaa sheria
ndogo ndogo ambazo zitatumika akuwabana wananchi ambao wanavitumia
vyandarua kinyume na ilivyokusudiwa
Alifahamisha kwamba
baadhi ya maeneo ya wilaya hiyo vyandarua vimezungushiwa bustani huku
baadhi wakivitumia kwa ajili ya uvuvi wa dagaa , jambo ambalo
linakwamisha ufanisi wamapambano dhidin ya malaria .
Akifunga kikao hicho
kwa niaba ya Afisa Mdhamini wizara ya afya pemba , dk Harouk Khalifan
hamad alisema mapambano dhidi ya malaria yanahitaji nguvu ya pamoja
kutoka wadau na wananchi wote .
katika zoezi la
ugawaji wa vyandarua kwa msimu huu jumla ya wananchi laki mbili hasini
na tisa elfu na mia nane thelethini na sita (259,836) ambapo
walioandikishwa ni wananchi laki nne sitini na saba elfu nan mia saba na
sitini na tatu (467,763) kwa kisiwa cha Pemba .
0 maoni:
Chapisha Maoni