posted by Esta Malibiche 22;23 KITAIFA
Halimashauri ya jiji la Mbeya huenda
ikashindwa kutekeleza agizo la Rais John
Pombe Magufuri, lililozitaka halmashauri kuhakikisha zinamaliza tatizo la
uhaba wa madawati shuleni ifikapo Juni 31, mwaka huu kutokanana kutokuwepo kwa msukumo
wa kutosha katika utekelezaji wa agizo
hilo.
Halmashauri ya Jiji la Mbeya,
imeweza kutengeneza na kukamilisha madawati 1500, wakati uhitaji ni madawati
10,000.
Katika upungufu huo, shule za msingi
zinauhitaji wa madawati 9894, wakati sekondari zikihitaji madawati 605.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa utengenezaji wa madawati katika chuo cha ufundi VETA jijini Mbeya ,
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji hilo, Mussa Mapunda, alisema katika madawati hayo 1500
ambayo tayari yamekamilika, madawati 798 ni ya shule za msingi huku madawati
477.
Alisema, kupatikana kwa madawati
hayo 477 kwa shule za sekondari halmashauri itakuwa imemaliza deni kwa upande
huo na kubaki na deni la madwati 9096 kwa shule za msingi ambao nayo yapo
katika mchakato wa kukamilika.
Akizungumza na baadhi ya wananchi wakiwemo
wanafunzi, madiwani na watumishi wa serikali, Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya,
David Mwashilindi, alisema madawati 9096 ambayo yanahitajika katika shule za
msingi yapo katika mchakato wa kukamilika.
Aidha, Meya huyo alisema, licha ya
halmashauri hiyo kukabiliwa na changamoto ya rasilimali fedha lakini imeweza
kufanya kazi hiyo kwa haraka hasa ukiangali ni kipindi kifupi tu, tangu kuungua
moto kwa mabweni zaidi ya mawili ya shule ya sekondari ya iyunga na kuteketeza
vitanda 150 na magodoro yake.
“Ninawashukuru wadau kwa kujitolea
kwani wakati wakichangia shule ya Iyunga, suala la madawati nalo likaingia
hivyo ninaamini kwamba halmashauri itaweza kukamilisha tatizo la madawati na
wanafunzi wote kuondokana na tatizo la kukaa chini,”alisema.
Mwisho.
0 maoni:
Chapisha Maoni