Uganda imeamua kuwaondoa wanajeshi wake kutoka nchini Somalia ifikapo mwezi Disemba mwaka 2017.
Uganda inachangia wanajeshi wengi zaidi kwa kikosi cha muungano wa afrika kinachopigana na wanamgambo wa Al-Shabab.
Mkuu wa
jeshi nchini Uganda Jenerali Katumba Wamala, aliiambia BBC kuwa hatua
hiyo ilichukuliwa kutokana na hujuma kutoka kwa jeshi la Somalia na
washirika wa kimataifa.
Marekani, Uingereza na Uturuki ni kati ya nchi ambazo hutoa mafunzo kwa jeshi la polisi wa Somalia.
Lakini serikali ya Uganda inasema kuwa nchi hizo hazitoi ushirikiano.
Jenerali
Wamala anasema kwa Uganda itaondoa jeshi lake kabla ya Disemba mwaka
2017 ikiwa nchi nyinge itapatikana kuchukua mahala pake.
0 maoni:
Chapisha Maoni