Wafanyakazi
wa kiwanda cha kuchapisha vitabu cha ABANA Printers ltd,kilichopo kata
ya Mapinga wilayani Bagamoyo mkoani Pwani,wakiandamana kudai mishahara
na mafao yao wanayodai kwa kipindi cha miaka miwili na nusu ambayo
yamefikia mil 400 .
(Picha na Mwamvua Mwinyi)
———————————————————–
———————————————————–
Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo
WAFANYAKAZI
wa kiwanda cha uchapishaji vitabu(ABANA Printers Ltd) kilichopo kata ya
Mapinga wilayani Bagamoyo mkoani Pwani ,wanadai fedha za mishahara na
mafao yao kiasi cha sh.mil.400 tangu mwaka 2014 bila mafanikio.
Aidha
wafanyakazi hao waiomba serikali ya awamu ya tano kuingilia kati tatizo
hilo kwani wameshapigania haki zao kupitia mahakamani ,wizara,idara na
vyama vinavyojishughulisha kutetea haki za wafanyakazi lakini hakuna
msaada walioupata.
Wameeleza
kuwa hadi sasa wanaishi katika maisha magumu huku wengine wakiwa
wamefukuzwa kwenye nyumba walizopanga na wenzao watatu wamefariki
kutokana na ugonjwa wa moyo.
Hayo
yamejiri jana baada ya wafanyakazi hao kuchukua hatua ya kufanya
maandamano nje ya kiwanda hicho na kisha kumfikishia kilio chao
mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi (CCM)Bagamoyo,alhaj Abdul Sharif ili
aweze kuwasaidia kulipwa haki zao.
Mwenyekiti
wa tawi la chama cha wafanyakazi tawi la ABANA printers Wilbard Ikigo
,alidai kuwa mmiliki wa kampuni hiyo anajigamba kwa kusema serikali ipo
mkononi mwake hivyo hawezi kuchukuliwa hatua yoyote.
Alisema
ni miaka miwili na nusu sasa tangu watelekezwe na mwajiri wao hali
iliyosababisha kuingia katika mgogoro na mmiliki huyo.
0 maoni:
Chapisha Maoni