Waziri
wa Kilimo, Maliaasili Mifugo na Uvuvi Hamad Rshid Muhammed, amesema ipo
haja kwa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika AU kuungana kwa pamoja
katika kuangalia soko la ndani katika masuala ya uvuvi ili kukuza uchumi
wa nchi hizo.
Akifungua
mkutano wa siku mbili wa Nchi wanachama wa Umoja wa Arika AU, wa
kujadili namna ya uzalishaji wa samaki, taaluma bora ya uvuvi na namna
ya kuwawezesha wavuvi, uliofanyika katika ukumbi wa Zanzibar Beach
Resort Mazizini, Hamad alisema soko la Afrika limekuwa likishuka
kutokana na kutokuwa na wataalamu wa kutosha katika sekta hiyo.
Alisema
mara nyingi nchi hizo zimekuwa zikijadili suala la kilimo kutokana na
kuonekana ndio muhimu kwa jamii, lakini sasa ipo haja kuzungumzia suala
la bahari kwa umuhimu wake hasa katika kukuza kipato cha wananchi na
taifa kwa ujumla.
Aidha,
aliwataka Waafrika kutumia fursa zilizopo katika nchi zao katika kukuza
uchumi wa nchi pamoja na kuwapatia wadau husika elimu itakayowajengea
uwezo wa kujua nyenzo ziliopo nchini ili waweze kufaidika nazo pamoja
kuwashawishi kutumia masoko ya ndani kwanza kabla ya kutumia masoko ya
nje.
“Tunalo
tatizo wenyewe sisi wa Afrika hatulitumii ipasavyo soko la
ndani,tunahangaika masoko ya nje wakati uchumi wetu wenyewe bado
haujakuwa, hivyo ipo haja kuungana wa nje na wa ndani ili tuweze kupanua
soko letu kwa matumizi yetu” alisema.
Nae
Mkuu wa Huduma za Wanyama na Mratibu wa Umoja wa Afrika, Simplece
Novala alisema madhumuni ya kufanya mkutano huo ni baada ya kuona tatizo
la soko katika samaki, ili kuweza kubuni njia zitakazosaidia kukuza
soko hilo na kujipatia ajira kwa wananchi katika nchi husika.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Maendeleo ya Uvuvi kutoka Tanzania bara,Fatma
Sobo alisema Tanzania bado ina tatizo kubwa katika masuala ya biashara
ya samaki, inatokana na kutokuwa na wataalamu wa kutosha, wavuvi waliopo
ni wadogo wadogo, vifaa duni walivyonavyo ambavyo wanachangiwa na
mabenki kuwanyima mikopo ya kuweza kujinunulia vifaa ili waweze kuvua
samaki wakubwa na kuongeza kipato kwa taifa.
Hivyo,
alisema kufanyika kwa mkutano huo hapa Zanzibar, utawasaidia kupata
elimu ya kutosha na kuwajengea uwezo wa namna gani wataweza kuboresha
huduma za msingi katika masuala mazima ya uvuvi.
Akizungumzia
biashara ya samaki ya ndani ya Afrika, Fatma alisema, bado Tanzania ina
tatizo la kuangalia zaidi kiwango cha samaki wanachopeleka nchi za nje
badala ya kuangalia samaki wa ndani, kwani jambo hilo linapelekea
kuonekana samaki wa ndani hawana ubora.
Meza kuu ikisikiliza utaratibu wa Mkuta kutoka kwa masta Solomon hayupo (pichani).
Sehem
ya wajumbe wa Mkutano wakimsikiliza mgeni rasmin Waziri wa Kilimo,
Maliaasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar Hamad Rshid hayupo (pichani)
alipokuwa akifungua Mkutano huo.
Mkurugenzi
kutoka Umoja wa Africa- Ofisi ya rasilimali wanyama Simplice Noula
akitoa tarifa ya ofisi yake katika Mkutano huo uliofanyika Hoteli ya
Zanzibar Beach Resort Mazizini Mjini Zanzibar.
Sehem
ya wajumbe wa Mkutano wakimsikiliza mgeni rasmin Waziri wa Kilimo,
Maliaasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar Hamad Rshid hayupo (pichani)
alipokuwa akifungua Mkutano huo.
Waziri
wa Kilimo, Maliaasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar Hamad Rshid Muhammed
akifungua Mkutano wa siku mbili wa mashauriano ya kitaalam juu ya
kuanzisha vituo bora vya uvuvi na ufugaji samaki Africa, uliofanyika
Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Mjini Zanzibar.
0 maoni:
Chapisha Maoni