SHELISHELI WAIHOFIA SERENGETI BOYS
Kocha
Mkuu wa timu ya soka ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ya
Shelisheli, Gavan Jeanne ameonesha kuihofia Serengeti Boys ya Tanzania
katika mchezo wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa
utakaofanyika Juni 26, 2016 kuanzia saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Jeanne alionesha hofu hiyo leo
Juni 25, 2016 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na mbele ya
Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Bakari Shime ambao kwa pamoja walikuwa
wakmizungumzia namna walivyoandaa timu zao kwa ajili ya mchezo huo wa
kesho.
“Hatujawahi kushiriki michuano ya
vijana. Hii ni mara yetu ya kwanza. Tumekuja kujifunza kwa wenzetu
Tanzania ambao wana uzoefu,” alisema Jeanne ambaye pia alithibitisha
kuwa hawajawahi kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa.
Kwa upande wa Bakari Shime wa
Serengeti Boys, alisema ameindaa mechi hiyo vema kiakili na kimwili kwa
ajili ya kuikabili Shelisheli katika mchezo huo ambao hamasa yake
imekuwa kubwa kwa kuwa kikosi hicho kinaandaliwa kuwa timu ya taifa
baada ya miaka miwili.
Wachezaji wa Serengeti Boys
wamesema, watafanya vema kwenye mchezo huo. Wachezaji hao ni Anthony
Shilole ambaye alisema: “Tumejifunza mambo mengi, ushindi ni lazima kwa
sababu tutafuata maelekezo ya walimu wetu. Tutajitahidi tushinde.”
Ally Ng’anzi: Maandalizi ni
mazuri. Mechi ya Jumapili tumejiandaa vema. Tunashinda tena kwa magoli
mengi.” Ally Msengi: “Watanzania watarajie ushindi baada ya maandalizi
ya muda mrefu. Timu iko kambini kitambo.” Kennedy Nashony: Tutapambana
kadiri ya uwezo. Kila mechi kwetu ni fainali. Hatuko tayari kupoteza ili
kukosa mechi zijazo.” Shelisheli ilitua Ijumaa usiku saa 7.45 usiku
ikiwa na viongozi 25 na imefikia hoteli ya Southern Sun iliyoko katikati
ya jiji la Dar es Salaam.
Waamuzi wanne kutoka Ethiopia,
ndio watakaochezesha mchezo huo. Waamuzi hao ni Belay Tadesse Asserese
ambaye ni mwamuzi wa kati wakati wasaidizi wake ni Tigle Gizaw Belachew
upande wa kulia na Kinfe Yilma Kinfe upande wa kushoto huku mwamuzi wa
akiba atakuwa Lemma Nigussie. Kamishna wa mchezo huo atakuwa ni Bester
Kalombo.
Serengeti Boys ilikuwa kambini
tangu Juni 14, 2016 kujiandaa na mchezo huo wa kufuzu fainali za Kombe
la Mataifa ya Afrika dhidi ya vijana wenzao wa Shelisheli utakaofanyika
Juni 26, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Mchezo
wa marudiano kati ya Serengeti Boys na Shelisheli utachezwa Julai 2,
2016 huko Shelisheli.
Katika kuajindaa na mchezo huo,
Serengeti Boys ilifanya ziara India ambako walishiriki mashindano ya
vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA (AIFF International Youth
Tournament 2016) kabla ya kurudi na rekodi ya kupigiwa mfano si tu
katika Tanzania na kwa nchi za Afrika Mashariki.
0 maoni:
Chapisha Maoni