Waziri
wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu
(katikati) akikagua majengo ya hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo Mjini
Dodoma,kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa hospitali Hiyo Profesa Ainory
Gessase.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu Profesa Ainory Gessase(mwenye koti jeupe)akimfafanulia
jambo waziri wa Afya wakati alipotembelea hospitalini hapo na kujionea
jinsi wanavyotoa huduma kwa wananchi
Waziri
Ummy Mwalimu akikagua baadhi ya vifaa tiba vilivyopo kwenye hospitali
hiyo ambapo zinahitajika shilingi milioni 137 za kitanzania kuweza
kufunga vifaa vya kiuchunguzi vya magonjwa ya moyo na figo.
…………………………………………………………………………………………..
Na.Catherine Sungura ,Dodoma
Serikali kupitia Wizara ya Afya
inatarajia kuzindua huduma zote Za kiuchunguzi za magonjwa kwenye
hospitali ya kisasa ya Benjamin Mkapa iliyopo mjini Dodoma
Hayo yamesemwa leo na waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati
alipotembelea hospitali hiyo na kuona inavyoendelea kutoa huduma za afya
kwa wananchi
Waziri Ummy alisema serikali
imejipanga katika kutekeleza ahadi yake kwa wananchi katika utoaji
huduma bora na za kisasa katika hospitali hiyo
“Nawaahidi nitafanya uzinduzi
rasmi wa huduma za uchunguzi wa magonjwa ili wananchi waelewe hospitali
yetu inatoa huduma zipi ili kila mwananchi atambue nini kinapatikana
hapa”alisema Mhe.Ummy
Aidha,Waziri Ummy alisema licha
ya kazi nzuri inayofanywa na watoa huduma wa afya wa hospitali hiyo
bado inakabiliwa na changamoto kubwa ikiwemo kukatika kwa umeme mara kwa
mara na kuahidi kuwasiliana na wizara ya Nishati na Madini ili kutatua
tatizo hilo.
Haha hivyo alisema wizara yake
inafuatilia upatikanaji wa fedha kiasi cha shilingi milioni 137 za
kukamilisha ujenzi wa ufungaji wa baadhi ya vifaa tiba vilivyopo
hospitalini hapo na hivyo kuwakaribisha wananchi wote kufika hospitali
hapo kupata huduma za kibingwa za ugonjwa wa kisukari
Mhe Ummy amesisitiza kuanza
kutolewa kwa huduma za vipimo (kama MRI na CT Scan) katika Hospitali
hiyo ili kuwapunguzia kero wananchi wa mikoa ya kanda ya kati kupata
huduma hizo Dodoma badala ya kusafiri hadi Dar es salaam kupata huduma
hizo.
Hospitali ya Benjamin Mkapa ipo
katika chuo kikuu cha Dodoma,kwa sasa inahudumia wagonjwa zaidi ya 170
kwa siku,ikikamilika itakua inafanya uchunguzi wa magonjwa ya
figo,kisukari pamoja na moyo
0 maoni:
Chapisha Maoni