Mashindano ya Copa America Centenario 2016 ambayo yamefanyika nchini Marekani yamekanilika kwa mchezo wa fainali kati ya Argentina iliyokuwa ikipambana na Chile.
Baada ya kumalizika kwa dakika 90 na zingine 30 za nyongeza timu hizo ziliingia hatua ya mikwaju ya penati na Chile kuibuka na ushindi kwa kupata penati 4-2 dhidi ya Argentina.
Mchezo huo uliokuwa wa kasi na timu zote zikishambuliana kwa kasi awali ulimalizika kwa sare ya bila kufungana na timu zote zikimaliza mchez huo kwa kuwa na wachezaji nusu uwanjani, mchezaji wa Chile, Marcelo Diaz akitolewa nje dakika ya 28 na Marcos Rojo wa Argentina akitolewa nje dakika ya 43.
Wachezaji wa Argentina waliopata penati ni Javier Mascherano na Sergio Aguero na waliokosa ni Lionel Messi na Lucas Biglia, kwa upande wa Chile waliopata ni Nicolas Castillo, Charles Aranguiz, Jean Beausejour na Gato Silva, aliekosa penati ni Arturo Vidal.