Jumatatu, 27 Juni 2016

KANISA LA EAGT LAKABIDHI MSAADA KWA WATOTO wanaotoka katika familia duni

Mkurugenzi wa Kituo cha Huduma na Mtoto EAGT Lumala Mpya, Jorum Samwel (kulia mwenye suti), akitoa ufafanuzi juu ya msaada wa vitanda, magodoro na vyakula uliotolewa na Kituo hicho ambacho kiko chini ya Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza.
Na BMG
Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba katika Manispaa ya Ilemela mkaoni Mwanza, limekabidhi misaada ya vitu
mbalimbali ikiwemo vitanda, magodoro na vyakula kwa watoto wanaotoka katika
familia duni ambao wanaolelewa na kanisa hilo.
Akikabidhi msaada huo hii leo, Askofu wa kanisa hilo Dkt.Daniel Moses Kulola, amesema watoto 18  waliokabidhiwa msaada huo ni sehemu ya watoto 264 wanaolelewa na kanisa hilo kupitia Kituo cha Huduma ya Mtoto iliyoanzishwa
kanisani hapo tangu mwaka 2010.
Askofu Dkt.Kulola amesema hiyo si mara ya kwanza kwa kanisa hilo kutoa msaada wa vitu hivyo na kueleza kuwa limekuwa
likifanya hivyo mara kwa mara ikiwemo kuwalea watoto hao kwenye maadili na afya njema na kuwaandaa kuwa watumishi wema katika jamii kwa baadae.
Nae Mkurugenzi wa Kituo cha Huduma na Mtoto EAGT Lumala Mpya, Jorum Samwel, amesema msaada huo umetolewa baada ya
uongozi wa Kanisa kuzitembelea familia hizo na kujionea hali duni za maisha wanayoishi ambapo baadhi yao hulazimika kulala chini baada ya nyumba zao kuathiriwa na mafuriko ya mvua yaliyotokea mwishoni mwa mwaka jana.
Wazazi, walezi na watoto walionufanika na msaada huo, wameushukuru uongozi wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya kupitia Kituo
cha Huduma ya Mtoto, ambapo wametanabaisha kwamba msaada huo utawasaidia kuondokana adha ya kulala chini iliyokuwa ikiwakabiri.
Msaada huo wa vitanda, magodoro, mashuka, mahindi na mchele umegharimu zaidi ya shilingi milioni tisa ambazo zilitolewa
na wahisani kutoka nje ya nchi ambapo wazazi na walezi wametakiwa kutambua
kwamba jukumu la kuwalea watoto katika maadili mema ni la jamii nzima badala ya
kuwaachia viongozi wa dini na taasisi za kijamii pekee.
Continue reading →

0 maoni:

Chapisha Maoni