Mkuu
wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues
amewakumbusha wadau wa urithi wa dunia na maeneo ya hifadhi kufanyakazi
kwa pamoja kwa lengo la kuhifadhi na kuyaendeleza maeneo hayo bila
kuondoa ushiriki wa wananchi wanayozunguka.
Kauli
hiyo ameitoa katika mafunzo yaliyoandaliwa na Shirika lake kwa wadau wa
mazingira ya hifadhi na urithi wa dunia mjini Marangu Moshi, kufuatia
makubaliano na serikali ya Tanzania.
Alisema
akizungumza na washiriki kwamba UNESCO inachofanya ni kuanzisha safari
ambayo inaweza kuwa ngumu na ndefu lakini washiriki wake ni lazima
kutambua namna ya kuendelea kufanya menejimenti ya maeneo ya hifadhi na
urithi wa dunia kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Akifungua
mafunzo hayo ambayo wataalamu ni washiriki wenyewe wakitumia njia ya
kuelewa ya methodolojia ya uchambuzi wa vikwazo (Bottleneck Analysis
Methodology) alisema safari ya kufanikisha menejimenti ya maeneo hayo
duniani na hasa hapa nchini ni yenye changamoto nyingi na kwamba wadau
wote wanatakiwa kuwa pamoja kuvishinda vikwazo hivyo na kuifanikisha
safari.
Mkuu
wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues
akizungumza katika warsha ya siku tatu iliyoandaliwa na shirika lake kwa
wadau wa mazingira ya hifadhi na urithi wa dunia iliyomalizika mwishoni
mwa wiki mjini Marangu, mkoani Kilimanjaro.
(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
—————————————
Akizungumza
katika warsha hiyo ambayo imechukua wadau mbalimbali wa masuala ya
urithi na menejimenti zake kutoka serikalini, taasisi zisizo za
kiserikali na wananchi wengine, alisema kwamba maeneo hayo yamezungukwa
na wananchi na pamoja na kuwawekea sheria za kutoharibu na kuyachakaza
ipo haja ya kushirikiana nao namna ya kupanga kuyaendeleza maeneo hayo
huku yakiwa yamebaki katika hali inayotakiwa.
Mafunzo
hayo yamelenga kuwajengea uwezo wa kupanga maendeleo katika maeneo
ambayo ni ya urithi wa dunia, binadamu na maeneo ambayo uhai unaweza
kuwepo.
Aidha
akifafanua zaidi mtawala huyo wa UNESCO nchini Tanzania amesema mafunzo
hayo yamelenga kuwapa wahusika nadharia zinazofaa katika safari ndefu
ambayo UNESCO nayo itashiriki na isingelipenda kumwacha hata mtu mmoja
nyuma.
Mafunzo
hayo yanatolewa kufuatia mpango wa UNESCO wa kutaka kuwa na uhakika na
kuhami maeneo hayo ya urithi; huku mamlaka zikitoa ushirikiano ili
kuwezesha malengo ya maendeleo endelevu, ambayo ndiyo ajenda ya dunia
kuelekea 2030, yanafikiwa bila kuathiri maeneo tajwa.
Ofisa
anayeshughulikia watu na maeneo yenye uhakika wa uhai: Biashara
zinazozingatia mazingira na uchumi unaombatana nao kutoka Sekta ya
Sayansi Ofisi ya Unesco, Dar es salaam, Myoung Su Ko akiwasilisha mada
kwa washiriki wa warsha hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Kilimanjaro
Resort mjini Marangu, mkoani Kilimanjaro.
Alisema
kwa kuwa kitaifa, serikali imeshatoa matamko ya kisera na kuweka
mikakati ya utekelezaji wa taratibu za kuhami maeneo ya kiutamaduni na
ya asili ipo haja ya wadau wengine kuona namna ya kufanyakazi kama timu
katika safari ambayo kila mmoja anastahili kuwaijibika kwa namna yake
hata kama kunatokea changamoto.
Alisema
wadau wanatakiwa kuangalia namna ya safari zao zinavyostahili kufanywa
na kuwa, kwa lengo la kutumia raslimali zilizopo kutekeleza mipango ya
maendeleo na ya kuhami maeneo hayo bila kutegemea msaada wa wafadhili au
wahisani.
Awali
katika ujengaji wa wazo la mafunzo ilielezwa kuwa pamoja na kuwapo na
juhudi kubwa za kuhami maeneo ya urithi wa dunia na kuyasajili maeneo
ambayo uhai unaweza kuwapo na wanadamu, kumekuwepo na changamoto kubwa
za maendeleo ambazo zinatishia kuvuruga mfumo tete wa ikolojia uliopo.
Katika
kufanikisha hifadhi ya maeneo hayo kumeonekana changamoto za upungufu
wa rasilimali watu wenye uwezo na vifaa vya kushughulikia uharibifu,
ukosefu wa uwezo wa kuhifadhi maeneo hayo kwa kuoanisha na uwapo wa
watu.
Mtaalamu
wa programu na utamaduni kutoka Ofisi za Unesco Afrika Mashariki Bi.
Karalyn Monteil akiwasilisha mada kuhusu makubaliano ya ulinzi katika
maeneo ya urithi na utamaduni wa dunia katika warsha hiyo iliyomalizika
mwishoni mwa juma mjini Marangu, Moshi.
0 maoni:
Chapisha Maoni