Jumapili, 26 Juni 2016

Habari kutoka vituo vya televisheni leo Juni 26


SIMU.TV: Rais Dr John Magufuli amezindua mpango  mkakati wa polisi katika kupunguza vitendo vya uhalifu nchini huku akilitaka jeshi hilo kuzingatia sheria na taratibu; https://youtu.be/9dzDjbTWnRo
SIMU.TV: Wakala wa barabara mkoa wa Mtwara TANROADS wamefanya zoezi la kuelimisha watembea kwa miguu sambamba na upandaji wa miti ili kutunza mazingira; https://youtu.be/OH8JWCrBSXI
SIMU.TV: Katika majiji yote matano nchini, Jiji la Mbeya ndio jiji linaloongoza kwa uchafu huku wananchi wakiitupia lawama serikali kwa kushindwa kufanikisha zoezi hilo; https://youtu.be/JJ5-Bgg3yug
SIMU.TV: Wakazi wa manispaa ya Mtwara Mikindani wamefanya usafi katika eneo la makaburi Msafa ili kuondoa vichaka ambavyo vilikuwa vinatumika kama maficho ya vibaka na wakabaji; https://youtu.be/rP01xfrfU18
SIMU.TV: Waumini wa kanisa la Mito ya Baraka kata ya Jangwani jana waliungana na waumini wengine Jijini Dar es salaam katika kufanya usafi ili kuunga mkono agizo la mkuu wa mkoa Paul Makonda; https://youtu.be/xfPE6Zam948
SIMU.TV: Mkurugenzi na mmiliki wa Gazeti la Dira Alex Msama amejitokeza mbele ya waandishi wa habari na kumuomba radhi waziri wa sheria na katiba Dr Harrison Mwakyembe baada ya kuchapisha habari inayomuhusu waziri huyo; https://youtu.be/Zy_ZjInDbUM
SIMU.TV: Wanafunzi wa shule za sekondari wilayani Maswa mkoani Simiyu wameshukuru mradi wa TASAF kwa kuwawezesha kusoma vizuri tofauti na hapo awali; https://youtu.be/Lh68PWda-cA
SIMU.TV: Joto la mchezo kati ya timu ya Taifa ya vijana Serengeti boys dhidi ya Shelisheli lazidi kupanda huku mchezo huo ukitarajiwa kuchezwa hii leo; https://youtu.be/EyJ2DA3Fa7E
SIMU.TV: Zaidi ya wachezaji 100 wamejitokeza hapo jana kushiriki mchezo wa Golf katika viwanja vya Golf vya Makongo;https://youtu.be/H8-Rq5EguqQ
SIMU.TV: Shirika la nyumba ya Taifa NHC limeanza kubomoa nyumba zake 9 mkoani Morogoro baada ya kushinda kesi yake ya msingi na wakazi wa eneo hilo; https://youtu.be/3NRvECEzwls  
SIMU.TV: Katibu mkuu wa TAMISEMI Mhandisi Mussa Iyombe amezitaka taasisi na halmashauri zitakazopokea fedha za uwezeshaji vijijini kuzitumia fedha hizo ili kuleta maendeleo; https://youtu.be/aYllL6IHji4
SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka amezitaka halmashauri zote mkoani humo kusitisha malipo kwa wakandarasi wote wa miradi ya maji; https://youtu.be/Ejg-Dr55EEQ
SIMU.TV: Watanzania wameaswa kutii maagizo ya viongozi wao hususani agizo la Rais Magufuli la kutaka kufanyika usafi kwa mazingira yetu; https://youtu.be/ERLNQiU9rZ4
SIMU.TV: Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema jukumu la kudumisha amani ni la kila mmoja wetu na kuwataka watanzania kudumisha amani kwa kuepuka vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani; https://youtu.be/m_qM1ip4oBk
SIMU.TV: Klabu ya soka ya Yanga imerejea nchini baada ya kuweka kambi takribani wiki mbili nchini Uturuki tayari kwa mchezo wao dhidi ya TP Mazembe siku ya Jumanne; https://youtu.be/lkzIwOg-rGo
SIMU.TV: Usaili kwa vijana wenye vipaji watakaoweza kushiriki katika shindano la Klabu Raha Leo Show linarushwa na TBC 1 & Taifa linazidi kushika kasi katika katika fukwe za Coco Beach; https://youtu.be/THbN1svgqlU
 

0 maoni:

Chapisha Maoni